Thursday, May 21, 2009

Dr. Harrison Mwakyembe apata Ajali ya Gari!

HABARI ZAIDI ZA AJALI ALIYOPATA DR. MWAKYEMBE LEO HUKO IRINGA!


Picha Kutoka JAMII FORUMS:
Shimo lililosababisha ajari ya Dr Mwakyembe
Dr Mwakyembe akifikishwa hospitali ya mkoa wa Iringa leo baada ya ajali

Gari la Dr Mwakyembe likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali

***************************************************************************


BREAKING NEWS (Kutoka ippmedia.com)

Mbunge wa Kyela, Dr. Harrison Mwakyembe amepata ajali ya gari leo asubuhi!
Nina tafuta habari zaidi!


*************************************************

MBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe amepata ajali mkoani Iringa karibu na eneo la Mafinga akiwa njiani akitoka Kyela kuelekea jijini Dar es Salaam, walioshuhudia tukio hilo wanaeleza kuwa gari la Dk Mwakyembe lilipata ajali baada ya kukwepa lori na kisha kutumbukia katika korongo ambapo tairi lilichomoka gari limeharibiwa vibaya na Dk Mwakyembe mwenyewe amekimbizwa hospitalini ambapo anaendelea na matibabu na anaweza kuzungumza kama, lakini haijajulikana ni kiasi gani ameumia.
Tutaendelea kuwaleteeni taarifa zaidi kadri muda unavyokwenda kuhusiana na maendeleo ya kiafya ya Dk Mwakyembe, ambaye amejitokeza siku za karibuni kukabiliana vikali katika vita dhidi ya ufisadi, vita vilivyomuingiza katika malumbano makali na wana- CCM wenzake pamoja na baadhi ya wafanyabiashara.

5 comments:

  1. Msiwe na wasiwasi. Dr Mwakyembe ameruka kama dk. 15 hivi zilizopita kuelekea Dar. Nilikuwa Uwanja wa Ndege wa Iringa maarufu kama Nduli Airport. Ni mwendo wa saa 1.00 hivi kwa ndege kutoka Iringa kwenda Dar. Hivyo wana JF wa DSM mnaweza kupiga jicho pale airport wakitua. Kutoka huku amesindikizwa na Dr. aitwae Nyabusani ambaye tangu alipoingia hospitali alikuwa akimhudumia. Tuna imani atafika salama na atapona haraka.

    ReplyDelete
  2. Yaap, tunajua nani kachimba hilo shimo!

    ReplyDelete
  3. Tunashukuru kwa taarifa ila mmedanganya kuhusu picha ni vyema mkawa wawazi badala ya kutafuta sifa ,hizi picha tumeanza kuzitazama mapema sana katika blog ya WWW.francisgodwin.blogspot wewe wasema zako huo ni wizi tena ni dhambi kubwa

    Salum Chuo kikuu cha Tumaini Iringa

    ReplyDelete
  4. Tunashukuru kwa taarifa ila mmedanganya kuhusu picha ni vyema mkawa wawazi badala ya kutafuta sifa ,hizi picha tumeanza kuzitazama mapema sana katika blog ya WWW.francisgodwin.blogspot wewe wasema zako huo ni wizi tena ni dhambi kubwa

    Salum Chuo kikuu cha Tumaini Iringa

    ReplyDelete
  5. Si ndio hao hao wanaofunga macho katika kukarabati mabarabara? Good lesson!

    ReplyDelete