Thursday, May 28, 2009

Nyanya Zamponza Da Veronica

Wadau, samahani lakini roho imeniuma sana nilivyona hizi picha. Yaani mtu anatafuta riziki kwa kuuza nyanya, halafu anayang'anywa! Na ninajua hao mgambo wanaenda kugawana bidhaa walizoiba! Ndiyo nimesema hao mgambo wameiba! Nilivyokuwa Tanzania mara nyingi nilishuhudia hao wanaojiita mgambo wakiwaibia machinga, mama ntilie na wengine mali yao! NANI ANAVUNJA SHERIA HAPO? Tanzania bado iko vile vile! Hao mgambo wafanye kazi ya kukamata vibaka na wezi waliozagaa juko mitaani na waache watu wanatafuta riziki kwa njia za heshima! Angekuwa CD wala wasingemsumbua!

*******************************************************************



Picha na Maelezo kutoka JIACHIE BLOG:

Mfanyabiashara wa nyanya katika soko la Kariakoo aliye fahamika kwa jina moja la Veronica akipambana na Askari Mgambo wa Jiji wakati walipokuwa wakichukua bidhaa zake ,kitendo hicho kimempelekea mama huyo kumwacha uchi jambo ambalo ni kinyume cha haki na sheria za binadamu.

JIACHIE inalaani vikali vitendo vya udharirishaji kama hivi,ambavyo kimsingi vinavuka mipaka ya haki na sheria za binadamu,hakuna mwenye haki ya kumvua nguo mwenzake hadharani,mbele ya watu lundo kama hivi.!

3 comments:

  1. Ifikie wakati waTanzania muwe na ufahamu wa kuweza kukemea vyombo ambavyo havina ustaarabu kama hii migambo.Leo imemtokea huyu dada lakini kumbuka kesho yawezekana ika wa ni wewe mbaya zaidi unaecheka.Kwani hawa ni maburudoza wanatumwa tu na wakija wala hawakuulizi.Tabia kama hii ikemewe sio kutuonyesha picha tu kama maonyesho kwani wamekuwa wakiwapa hasara sana wafanyabiashara wadogowadogo.

    ReplyDelete
  2. AIBU! Yaani mgambo hawana kazi zaidi ya kusumbua akina mama wanaotafuta riziki yao!

    ReplyDelete
  3. haya ni mambo ya kawaida tu katika nchi yetu inayoongozwa na serikali ya CCM! Hii ni mojawapo wa picha nyingi sana za unyanyasaji wa vyombo vya dola dhidi ya wananchi. Hao ni wafanyabishara ambao wanalipa kodi na kupiga kura, lakini hotolewa kwa nguvu nyingi na bidhaa zao kuporwa na askari hao wa jiji! Wananchi tukiwa tumebaki tumeduwaa tukiangilia tu!
    du! kwa kweli, Kila mtu na msalaba wake!

    ReplyDelete