Friday, June 12, 2009

Serikali Yaondoa Ushuru wa Kamera

ASANTE SANA RAIS WETU MPENDWA JAKAYA KIKWETE!

*************************************************
Kutoka ippmedia.com
Serikali yaondoa ushuru wa Kamera

Na Mwandishi wetu

12th June 2009

Serikali imeondoa ushuru wa forodha kwenye kamera maalum za kupiga picha za filamu ili kuhamasisha sekta ya filamu kwa nia ya kuongeza ajira na kipato kwa vijana hapa nchini.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkullo wakati akisoma bungeni mjini Dodoma bajeti ya mwaka 2008 na 2009. Kwa mujibu wa Mkullo, kamera hizo zilizofutiwa ushuru ni zile maalum za kupiga picha za filamu zinazotambuliwa chini ya HS Codes 8525.80.00.

Hatua hiyo ya Serikali ya kuondoa ushuru imekuja baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Mrisho Kikwete kukutana na watengenezaji na wacheza filamu wa Hollywood wakati alipotembelea Marekani kwa ziara ya kikazi.

Sekta ya filamu hapa nchini imekuwa ikipanda chati kwa haraka sana, ambapo vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na shughuli za uchezaji na utengenezaji wa filamu mbalimbali.

Hatua hiyo ya Serikali itasaidia wawekezaji kuja nchini kuwekeza katika sekta hiyo kama sekta nyingine na kuinua fani hiyo ambayo ilikuwa chini sana.

2 comments:

  1. Mwalimu Nyerere alisema kutengeneza filamu ni anasa. Matokeo tumepoteza sehemu kubwa ya historia yetu imepotea na hatuna sinema nyingi kutoka 1960's hadi 1990's kutuburudisha zaidi ya zilizotoka abroad. Hongera Rais Kikwete kwa hatua uliyochukua.

    ReplyDelete
  2. Hatuna focus, Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

    Lakini, makampuni na mashirika mengi ya teknolojia na habari makubwa duniani yanatambua kuwa ukitaka kuendesha mradi wa Kiswahili kwa mafanikio na ushirikiano wa serikali na wadau nenda Kenya....


    Tujiulize, kama lugha ni yetu kwanini hatuna cha kunufaika zaidi ya kuizungumza?

    Tulitakiwa tuwe trailblazers katika kukitumia Kiswahili kwa manufaa ya kitaalam na kiuchumi.

    Ndiyo yale yale, Tanzaninite inapatikana Tanzania, lakini Kenya ndiyo muuzaji mkuu katika soko la kimataifa.

    Viongozi wetu hawana vision ya kuinyanyua Tanzania, wanatumia muda mwingi kuwabana CHADEMA na CUF badala ya kujipanga kushindana na Kenya na Rwanda.

    Utakuja kusikia wataalam wa Kiswahili wanatoka Rwanda kwenda kutoa mafunzo ughaibuni na sisi tumebaki kupokonyana majimbo katika uchaguzi mdogo.

    Mifano tu ni Microsoft, Google, Facebook, BBC, China Radio International.

    ReplyDelete