TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara kama ifuatavyo kwa lengo la kujaza nafasi zilizokuwa wazi pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi kwenye Wizara kama ifuatavyo:-
1. Bwana ELIAKIM CHACHA MASWI - ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) atakayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kabla ya uteuzi huo, Bwana Maswi alikuwa Kamishna Msaidizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha na Uchumi.
2. Bwana JUMANNE ABDALLAH SAGINI – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI atakayeshughulikia Elimu ya Msingi na Sekondari. Kabla ya uteuzi huu Bwana Sagini alikuwa Mratibu wa Mradi wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
3. Dr. SHAABAN RAMADHANI MWINJAKA – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko. Kabla ya uteuzi huu Dr. Mwinjaka alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Makamu wa Rais.
4. Bi. ELIZABETH JOKTAN NYAMBIBO – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huu Bi. Nyambibo alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.
5. Bwana ULEDI ABBAS MUSSA – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Bwana Mussa alikuwa Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji kwenye Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
6. Dr. PATRICK S. J. J. MAKUNGU – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Kabla ya uteuzi huu Dr. Makungu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa ‘Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology’, Arusha.
Uteuzi huu unaanza tarehe 13 Juni, 2009.
(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI
IKULU,
DAR ES SALAAM.
23 JUNI, 2009
No comments:
Post a Comment