Saturday, August 08, 2009

Jaji Sonia Sotomayor Kuapishwa Leo

Leo jambo la kihistoria itatendeka Marekani. Jaji Sonia Sotomayor ataapishwa kuwa 'Justice' katika mahakama kuu ya Marekani (Supreme Court). Anachukua nafasi ya Jaji David Souter ambaye anastaafu.

Kuapishwa kwa Mama Sotomayor ni jambo la kihistoria kwa sababu ni Mspanish. Anakuwa jaji wa kwanza mspanish katika mahakama hiyo. Takwimu zinasema kuwa mwaka 2050 idadi ya waspanish Marekani itazidi wazungu. Lakini ajabu hali yao ni duni katika elimu Marekani, tena kuliko weusi.

Mama Sotomayor aliteuliwa na Rais Barack Obama, ambaye ni rais wa kwanza mweusi Marekani. Kitendo chake cha kumteua kitasaidia uhusiano kati ya waspanish na weusi Marekani. Sehemu nyingi weusi na waspanish hawpendani kabisa ingawa wote wanaonewa na wazungu.

Pia Mama Sotomayor atakuwa mwanamke wa tatu kuwa jaji katika Supreme Court.

Hongera Justice Sonia Sotomayor.

1 comment:

  1. Sasa wewe unatuchanganya hivi hawa spanish sio wazungu?ongea mzungu anayetoka espania sio eti wazungu wanawaonea,,sema wamarekani wanawaonea waspania kama watu weusi.

    ReplyDelete