Sunday, September 13, 2009

Caribbean Festival Kwetu Cambridge Leo! Part II

Mara parade ilivyoisha hawakuchelewa kuanza usafi!
Kulikuwa na polisi kibao kutulinda! Bila shaka mmesikia habari za fujo wanazofanya kwenye hiyo parade wakiwa Boston, hata watu wamepigwa risasi na kuchomwa visu, na hata kufa. Kwetu Cambridge, mambo shwari! Tatizo hao wanaume wanaolinda wanawake zao kwenye parade. Umtizime GF au mke wa mtu utakoma! Wanaume wao wako karibu! Lakini wengine wako karibu uchi utaweza kuacha kuwtazama kweli?
Hao walipita kwenye sidewalk, maana hawakuwa official. Walikuwa wananuka bangi, ile mziki wao ulinikumbusha muziki wa asili ya waKulya.




Nimeshika bendera ya Jamaica, ni nchi alikozaliwa mama yangu. Huyo baba sijui nitammwona wapi nimpe picha yake!

Huyo baba alikuwa amelewa. Alikuwa anasakata rhumba, alisema yeye ni mzuri wa ajabu (Most handsome Man) na wanamwita Denzel Washington au Billy Dee Williams. Jirani yangu anayetoka Jamaica kamwambia, "don't kid yourself!" Alisema anatoka Trinidad.

Huyo jamaa alichukua bendera yangu, aliomba apige picha nao. Alikuwa amelewa mno, na kaongea lugha ambao sielewi!

Hao wameikumbusha ngoma ya Sindimba!



Huyo dada alihangaika mno na hiyo costume. Mpaka tukapiga bets kuwa hata fika mbali kwa maan ilikuwa nzito na alikuwa hoi! Alivyofika mbele yetu kwenye taa walimpa mtu mwingine aivae! Huyo alikuwa karibu kuzimia!

Hao walichelewa na walikuwa wanaenda kujiunga na wenzao.

3 comments:

  1. Chemi,
    ulibeba bendera ya Jamaica?Kwani wewe ni mjamaica?

    ReplyDelete
  2. Kama nilivyosema, mama yangu anatoka Jamaica na nina ndugu kibao huko.

    ReplyDelete
  3. Hiyo mi costume ni mzigo. Nahisi inbidi ushibe haswaa ndio uvae.

    ReplyDelete