Monday, November 09, 2009

Kivutio cha Watalii kijijini Manda


Wadau, hii kaburi ni la Mjerumani aliyekufa huko Manda mwaka 1904. Alizaliwa 1879. Maandishi yalikuwa kwa kijerumani hivyo sikuelewa vizuri wanasema nini. Nasikia wazungu wakifika kijijini ni lazima wafike huko kuona kaburi. Ni njiani kwenda kanisa la St. Thomas, huko Nsungu. Pia watu huko wanaamini kuwa wajerumani wameacha dhahabu tele huko kijijini. Kila siku watu wanachimba huko kuzitafuta!
Stori inaendea hivi, Mwingereza alipovamia, wajerumani walitia dhahabu yao kwenye sanduku. Waafrika wawili walipewa kazi la kubeba hiyo sanduku. Waliambiwa wachimbe shimo kubwa la kuficha hiyo sanduku. Baada ya kuchimba hilo shimo, waliingiza sanduku. Wajerumani waliwapiga risasi hao waafrika wawili na kuwazika humo humo kwenye shimo na hilo sanduku la dhahabu. Walihofia watasema wameficha wapi hiyo dhahabu. Kuna watu ambao wanaamini kuwa wajerumani wameacha ishara kadhaa kuonyesha walipozika ila sanduku.
Picha zingine zitabandikwa kesho jioni.

8 comments:

  1. Dada Chemi, hichi kijiji kinaitwa Nsungu (ikiwa na maana Mzungu), siyo Isungu. Mimi pia natokea mitaa hiyo.

    ReplyDelete
  2. Anonymous wa 5:30am, asante sana kwa sahisho. Naomba unisaidie correct name ya mlima maarufu wa Manda. Sijui ni Likulumbula, Likulumbola.

    ReplyDelete
  3. Monile chemi!
    Jamani wewe chemi umenitoa machozi na mimi ni kwetu uko baba yangu latokea kijiji cha Lundu na mama yangu katokea kijiji cha mbaha uko nsungu nina dada zangu wameolewa uko.
    Mwengaaaaaaa chemi nitafute dada yangu mimi nipo hapa spfld,ma ukute mimi ni mapunda umenikumbusha mbali na hiyo bandari maana nilikwenda uko 2005.

    ReplyDelete
  4. Monileeee chemi!
    Jamani wewe chemi umenitoa machozi na mimi ni kwetu uko baba yangu latokea kijiji cha Lundu na mama yangu katokea kijiji cha mbaha uko nsungu nina dada zangu wameolewa uko.
    Mwengaaaaaaa chemi nitafute dada yangu mimi nipo hapa spfld,ma mimi ni mapunda umenikumbusha mbali na hiyo bandari maana nilikwenda uko 2005.

    ReplyDelete
  5. wee chemi vipi? unaweza kuspeli "kaembrij masaschuses" lakini huwezi kuspeli "Nsungu"? taratibu dada

    ReplyDelete
  6. Dada Yasinta, aise hata mi imenikumbusha mbali sana hii kitu, yaani kunyumba....Nilikuwa kwenye hiyo bandari Nsungu mwaka 2002,
    magono giluta....mwengaaa.duh.

    ReplyDelete
  7. kweli milima haikutani watu hukutana. huyo mukeshi(Mtoto wa Bwana Boga) kasoma uyui sec na Nyumbani kwao ni Ng'ambo (Kwihara St)Baba yake ni muhindi.Kweli bado mnakumbukana mnatoroka Tabora girls mnapitia Kwa boga kulikuwa wanachomea maiti na makaburi ya wahindi.
    Nitakuletea kumbukumbu za Warsal,Nato,Paris na Berlin kaa standby Ba'Sablati

    ReplyDelete