Friday, November 13, 2009

Kuchimba Dawa Safarini Mkoani

Siku hizi Tanzania kuna tangazo kwenye TV la TIGO. Jamaa yuko kwenye basi ya mkoani kwenda songea. Wanasimama kuchimba dawa na yeye anaachwa. Anamtumia jamaa text message kwenye basi na wanamrudia.

Kwenye basi la kwenda Kyela, tulisamama mara kadhaa ili watu waweze kuchimba dawa. Tulisamama Kitonga Mountain Resort, kwenye kituo cha mafuta na kuna vituo vya kuchimba dawa porini. Chini ni picha ya kituo fulani huko Iringa. Mnashuka mnaingia bush. Hebu ona toilet paper zilivyozagaa.





3 comments:

  1. watanzania hatujui kutumia fursa zilizopo. kuchimba dawa kwa namna hii ni fursa ya kibiashara. ghana wanafanya na wameweza. sie wizi tu.

    kwa mfano sehemu kama hii ya kuchimba dawa pale morogoro baada ya kuiacha morogoro town ni sehemu iliyoshamiri biashara ndogongogo. wafanyabiashara hawa nawaita wabunifu. muuza vocha mmoja nilishangaa ananitolea chenji miongoni mwa manoti yanayokaribia ama kuzidi milioni 2.

    sasa badala ya kuharibu mazingira kiholela serilkali ingeweka agizo kuwa watu wawekeze vyoo mathalani 30 hivi visafi. au hata serikali yenyewe ijenge si tushazoea ujamaa. halafu wamachinga waandaliwe vijisehemu maalumu (stalls). serikali zitafaidika kwa kumchapa kodi mwekezaji, kuwachapa kodi wamachinga, kutunza mazingira kwa sababu kwa sasa huo ni uchafuzi wa mazingira. hebu angalia jangwa linavyonyemelea hapo. halafu ingekuwa marufuku kwa mabasi kusimama sehemu nyingine yeyote kwa madhumuni hayo isipokuwa kwa dharula maalaumu kama tumbo la kuhara la abiria. tena ili kupata mijihela ningewashauri:

    dar- moro- kituo kimoja
    moro - mikumi kituo kingine
    mikumi-iringa - kituo kingine
    iringa- makambako -kituo kingine
    makambako-mbeya - kituo kingine

    ReplyDelete
  2. MMMMMmmmmm dada Chemi kweli umetuletea mambo ya msingi kuyatafakari kwa kina.Unajua dada watu wamejaa na mawazo ya kuchukia Ufisadi lakini hali ya uchafuzi wa mazingira hawana habari nayo.Hata profesa Mwakyusa anapita njia hiyohiyo wala hashtuki kabisa juu ya afya za watu.Kama sikosei mwaka jana nilifanya safari ya kwenda Tanzania na nikatinga Mbeya hadi Tukuyu home.Hapo ambapo mabasi yanasimama na watu wanachimba dawa ni mahali hapohapo watu wanauza vyakula na minyama choma kibao.hebu fikiria mazingira ndiyo hayo na bado hapo hapo ni hoteli bandia.Hii kali jamani.

    Dada Chemi asante sana kwa kutudindua bila shaka sasa tuanze kulijadili na kulitupia macho hili suala kuchimba dawa katika vichaka.

    Umenifurahisha sana kwa safari yako hiyo wewe mdada.

    ReplyDelete
  3. John Mwaipopo umesema vizuri sana kwa kweli kama ingefanyika hivyo ingeleta maana sana na kujenga heshima ya watu pia maana hii ya kunya na kukojoa hovyo haifai kabisa.Ukiwa kwenye basi watu wakitelemka ukiangalia huko vichakani unaona tu watu kina mama kina dada wanapenbjua nguo wanajisetiri hii ni kuwatia watu aibu kabisaaa maana hawana jinsi wafanyeje.Hebu Mwaipopo pasha habari hii huko maana wewe ni mwandishi wa habari.wambieni kaka yetu Mwakyusa alifikirie hilo kwa afya ya binadamu.

    ReplyDelete