Wednesday, November 18, 2009

Sinema - Precious (PUSH: Based on the Novel by Sapphire)


Wadau, jana nilienda Loews AMC Boston Common kuona sinema, Precious. Ilikuwa Advance Screening kiingilio bure. Kwa bahati mbaya nilishindwa kuingia kwani nilikuwa kati ya watu zaidi ya 1,000 waliorudishwa kwa vile ukumbi ulikuwa umejaa. Watu walifika pale saa 9 mchana, na screening ilikuwa saa moja. Nilifika pale saa 12 kasorobo na mamia ya watu walikuwa wanarudhishwa! Walisema waliofika hiyo saa 9 walikuwa wengi mno na kujaza ukumbi!
Watu wamekuwa wakingoea kuona hii sinema kwa zaidi ya mwaka moja! Stelingi wake ni Mo'nique na mgeni katika sinema, Gabourey 'Gabby' Sidibe. Inahusu maisha ya msichana mwenye miaka 16 aliyebakwa na baba yake na kuzaa watoto wawili huko Harlem, New York mwaka 1987. Kwa vile ni mweusi tii na mnene anaona kama hana thamani duniani. Gumzo ni kuwa sinema ni nzuri mno na huenda stelingi wake na sinema enyewe itapata tuzo ya Oscar.
Ijumaa wiki hii sinema itaonyeshwa katika sinema kadhaa hapa Marekani. Nitaenda kuangalia na kuwapa maoni yangu.

8 comments:

  1. Nasikia ni nzuri sana. Naona huyo Gabby atapata Oscar kama Jennifer Hudson.

    ReplyDelete
  2. Nilikuwa namsikiliza DIRECTOR wake kwenye Tell Me More ya NPR. Alivyofafanua naamini nitaenda kuiona. Ameeleza mengi mema na namna mfumo mzima wa maisha usivyowapa nafasi ya pili wasichana wadogo wanaopata mimba na kukacha shule kutunza familia zao changa.
    Nimependa maelezo yake na naamini nitaweza kwenda kuiona
    Asante kwa kutushirikisha haya.
    Blessings

    ReplyDelete
  3. Da chemi,
    Sinema yoyote inayokandia black people whether is based on true story au fiction lazima actors or actress wake wapate awards, this movie is so degrading to black people as a whole ingawa sisi africans we dont dont consider ourselves as black americans here in america, you know what am talking about. so hakuna jipya is just enforcing the existing stereotypes.

    ReplyDelete
  4. mweusi tii maana yake ni nini?

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 9:36pm, I agree. Hii sinema inapendwa sana na wazungu maana inaonyesha mweusi akiwa chini kabisa. Yaani ni stereotypes wanazojua. Katika hii sinema weusi wana tabia chafu kuliko wanyama mfano, mtu kutembea na mwanae! Itapata tuzo kibao. Ingehusu familia ya wasomi, maisha yao mazuri wala msingesikia kitu. Hata hivyo ninashukuru kuona sinema ya weusi inashabikiwa hivyo, pia Mo'nique na Gabby wanafungua milango kusudi actors kama mimi tupate nafasi kuigiza katika sinema za Hollywood.

    ReplyDelete
  6. yes.....kama Halle Berry alifunua uchi wake kwa Billy Bob Thorton Kwenye Monsters Ball alipata Oscar na Denzel alivyo act kama a bad cop pia alipata Oscar....kuana movie nzuri tuu wamewahi kuact watu hawa lakini hawakuziconsider!!!!

    ReplyDelete
  7. Mdau 6:04. Mweusi Tii manake PITCH BLACK.

    ReplyDelete
  8. Mimi sikubaliani na Mdau wa 9.36 na pia dada Chemi. Najua kuna stereotype hasa linapokuja suala zima la mtu mweusi kuonyeshwa katika hali ya chini kabisa. lakini kuna kitu ambacho ningetaka kusema, hivi vitendo vichafu vipo katika jamii ya weusi. Nafikiri sinema si kwamba inaonyesha mtu mweusi katika hali ya chini, lakini pia inaonyesha na kuelezea tatizo lililopo katika jamii ya watu weusi. Na hii inakuwa tatizo sisi kuelewa kwani mara nyingi watu weusi huwa hatukubali tatizo zaidi ya kulalamika tu. Kwa mfano katika jamii yetu msichana akibakwa au akifanyiwa mambo mabaya utaona watu wanasuluhusha tu kwani huwa inaoneka ni aibu kwa jamii badala ya kuonekana ni tatizo.

    Suala la kushabikiwa sana na wazungu hapo sijaelewa labda mfafanue zaidi ni kwa nini inashabikiwa sana?

    ReplyDelete