Thursday, December 10, 2009

Mzungu Amtemea Mate Trafiki Dar!

Hapa Marekani zamani wakati ubaguzi ulikuwa waziwazi ilikuwa jambo la kawaida mzungu kumtemea mate mtu mweusi. Lakini jamani wazungu wanafanya hivyo Afrika, huko wanakuja kwetu kuishi kwa anasa ambazo hawawezi kupata kwao! Kwa kweli nimechukia kusikia habari hizi! na hebu wafanya DNA ya hiyo mate wampige persona non grata Tanzania!

**********************************************************************

kutoka ippmedia.com

Mzungu amtemea mate trafiki Dar
Na Moshi Lusonzo
10th December 2009


Mzungu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mfanyakazi wa ofisi ya ubalozi wa Canada nchini hapa, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumtemea mate askari wa usalama barabarani (Trafiki) aliyekuwa akiongoza magari, Jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema tukio hilo la aina yake lilitokea jana saa 8:15 mchana eneo la Ukonga Banana, barabara ya Nyerere Jijini.

Kamanda amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Gean Touchatte, 48, ambaye imeelezwa kuwa ni Katibu Mhitasi wa ubalozi huo.

Akisimulia tukio zima, Kamanda Shilogile amesema kabla ya tukio hilo, trafiki mwenye namba NCO E1653 Koplo Samson, alikuwa kazini akiongoza magari katika barabara ya Nyerere pale Ukonga Banana.

Akasema wakati huo mtuhumiwa huyo alipita akiendesha gari lenye namba za usajili T 17 DC 178 aina ya Toyota Land Cruiser, akitokea Ukonga kwenda Uwanja wa Ndege.

Kamanda Shilogile amefafanua kuwa mtuhumiwa huyo alipomkaribia trafiki, alipunguza mwendo, akashusha kioo cha gari, kisha akamtemea mate askari kabla ya kuongeza mwendo na kuondoka.

Kwa mujibu wa Kamanda Shigolile, trafiki alitoa taarifa za tukio hilo kwa wenzake kupitia `redio call’ za polisi, juhudi zilizosababisha gari hilo kufuatiliwa.

Amesema gari lilipofika maeneo ya Kamata, lilikamatwa na askari na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Kamanda amesema wakati mtuhumiwa huyo akiendelea kuhojiwa kituoni hapo, alifika mwandishi wa habari wa TBC, Jerry Muro akiwa na nia ya kumhoji lakini naye inadaiwa aliishia kutemewa mate yaliyompata chini ya kidevu na kuenea upande wa mbele wa fulana aliyokuwa amevaa.

Amefafanua kuwa kutokana na kitendo hicho, mwandishi huyo alifungua jalada la mashtaka ya shambulio kituoni hapo na kufunguliwa jalada namba CD/102/4818/2009.

Kwa mujibu wa Kamanda Shilogile, mtuhumiwa huyo hakuwa tayari kutoa maelezo yoyote, kwa madai kuwa atafanya hivyo pindi akiwepo balozi wa nchi yake.

Aidha, akasema fulana ya mwandishi Jerry Muro iliyotemewa mate, imehifadhiwa katika Kituo cha Polisi Kati kwa ajili ya ushahidi na mtuhumiwa huyo anaendelea kushikiliwa na Polisi.

8 comments:

  1. Kesho utasikia amerudishwa kwao Canada. Huenda wacanada watampa huyo polisi scholarship kama fidia. Bahati ya huyo trafiki.

    ReplyDelete
  2. ni kweli atarudishwa kwao si bado tunawaona ni miungu watu!!ila kwa vile alimtemea mate na mwandishi wa habari ,alipokuwa anahojiwa na BBC alidai atasimama kidete kuhakikisha haki inatendeka mimi binafsi na muunga mkono kwa hilo.Ila tuombe mungu huyu mwandishi asizibwe mdomo.
    Tusubiri tuone!!!!

    ReplyDelete
  3. Enzi za mchonga, huyo angesindikizwa Airport baada ya kupewa notice ya masaa tu. Na angetakiwa asikanyage. Pia huenda tungeandamana vile?! sikumbuki vizuri. Anyway, ndiyo hivyo.

    ReplyDelete
  4. Bahati? Kupata scholarship kwa kutemewa mate ni bahati??? Are you real my Friend?????

    ReplyDelete
  5. Enzi za Mwalimu, huyo mzungu angekwisha kuwa declared 'persona non grata' na kurudishwa Canada. Angeambiwa asije Tanzania tena. Wazungu wengi walirudishwa hivyo, wao wa mbwa, walio kuja kama walimu na kutembea na wasichana wa shule, walioua!

    ReplyDelete
  6. FUKUZA MBALI HUYO MZUNGU MSHENZI!

    ReplyDelete
  7. Kumtemea mate Askari ambaye ni mtumishi mheshimiwa wa serikali, ni matusi makubwa. Huyo mzungu, asingethubutu kitendo hicho angekuwa yuko kwao au nchi yeyote ya Magharibi (Ulaya) ni dharau kubwa na sio ya kuchukuliwa kimchoro-mchoro. Tunataka kuona adhabu yeyote au kuona msamaha waki hadhara kwenye televicheni na habari magazetini.
    Sheria za ki-diplomasia pia zi angaliwe tena na kubadilishwa, kwa maana kitendo hicho kisingechukuliwa juu-juu kwenye inchi yetote duniani, kwa nini sisi tunalegeza na kufwata hizo sheria. Huyo Askari ni mtumishi wa serikali ni lazima swala hili lichukuliwe kwa uzito unaotakiwa na atetewe na nchi yake.

    Tafadhali tuwaheshimu watumishi wetu kwa kuwasimamia kijasiri, kitendo hicho kitatupatia heshima katika nchi yetu na msimamo. Ni lazima hilo lizungu liadhibiwe.
    Anna. Uk

    ReplyDelete
  8. jamani jamani jamani... roho imeniuma sana.... hiyo ni dharau ya ajbu... mshenzi huyo nipo huku kwao wana dharau pia huko kwetu? tena polisi? how abt raia wakawaida? plz ashughulikiwe kikamilifu huyo mshenzi,kama ni mbaguzi anaona kichefuchefu arudi kwao....naomba serikali msiishie hapo itakuwa dharau kubwa labda apimwe ijulikane ni mwehu ndo aachwe...but kama mzima onyesheni mfano kwa wenzake plzzzzzzzzzzzzz

    ReplyDelete