Kutoka ippmedia.com
11th January 2010
Wananchi wakitoa damu kwa ajili ya kupima virusi vya ugonjwa wa Ukimwi
Matumizi makubwa ya fedha kupambana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi Mkoani Iringa, bado hayajasaidia sana kutokana na takwimu za sasa kuonyesha kwamba maambukizi hayo hivi sasa yamepanda hadi kufikia asilimia 24.5.
Tofauti na sasa, takwimu za mwaka 2007/2008 zilionyesha kwamba maambukizi ya ukimwi mkoani Iringa uliokuwa ukiongoza kitaifa yalikuwa asilimia 15.7. Iringa ilikuwa ikifuatiwa ‘kwa karibu’ na Mikoa ya Mbeya na Dar Es Salaam.
Takwimu hizo za kukatisha tamaa zilitolewa katika kikao maalum cha kupitia utekelezaji wa mkakati mpya wa miaka minne wa Mkoa wa Iringa wa kupambana na ukimwi, kilichofanyika Makambako, wilayani Njombe Mkoani hapa.
Taarifa zilizowasilishwa katika kikao hicho zinaonyesha kuwa, matokeo ya upimaji wa virusi vya Ukimwi kwa hiari kati ya Julai 2008 hadi Juni 2009 yalionyesha kwamba, mambukizi ya virusi vya ukimwi hivi sasa ni asilimia 24.5 ingawa upimaji huo hauwakilishi sampuli za mkoa mzima.
Takwimu hizo za sasa zilionekana kumkera Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Aseri Msangi, ambaye alisema inashangaza kuona kwamba kasi ya maambukizi hayo inaongezeka wakati mkoa na wadau wake wanapata fedha nyingi zaidi kwa ajili ya mapambano yake.
“Inakuwaje kadri tunavyotumia fedha nyingi zaidi ndivyo maambukizi yanavyozidi kuongezeka… Kwa nini?” alihoji Mkuu huyo wa wilaya ingawa hakukuwa na jibu la maana kutoka kwa watendaji zaidi ya kurudiwa kwa vyanzo vya maambukizi kama mila potofu, ngono zembe, kurithi wajane na ulevi.
Oktoba 2008, Mkoa wa Iringa ulizindua mkakati wa miaka minne wa kupambana na ukimwi ambapo hadi Oktoba 2009, Mkoa pamoja na wadau wengine ulitumia Sh. bilioni tatu katika kupambana na maambukizi hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Charles Gishuri pia alionyesha kutoridhishwa na utendaji wa Mkoa na wilaya katika mapambano hayo.
Katika kila dalili zinazoonyesha kuwepo kwa ufisadi wa fedha za ukimwi Mkoani Iringa, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Getrude Mpaka, alitoa taarifa iliyoshtua wengi kwamba tangu achukue wadhifa huo mkoani hapa, hajawahi kupata taarifa yoyote ya maandishi ya Kamati ya Ukimwi ya Mkoa ikieleza jinsi inavyoratibu mapambano dhidi ya janga hilo.
Takwimu za sasa zilionyesha kwamba wilaya inayoongoza kwa kuwa na kasi kubwa zaidi ya maambukizi ni Makete yenye asilimia 35.9, ikifuatiwa na Njombe yenye asilimia 31.9 na Iringa yenye asilimia 30.5.
Zingine na kiwango chake cha maambukizi kwenye mabano kutokana na matokeo hayo ni Mufindi (asiliamia 24), Manispaa ya Iringa (asilimia 23.5), Njombe Mjini (asiliamia 21.1), Ludewa (asiliami 18.6) na Kilolo ni ya mwisho kwa kuwa na asilimia 12..2.
Mchungaji Ebron Misitu wa KKKT Ludewa alisema katika kikao hicho kwamba kama kutakuwepo na uaminifu wa matumizi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya mapambano hayo, njia ya mafanikio pia itaonekana.
CHANZO: NIPASHE
tamu sana kutazama,
ReplyDeleteute wanichuruzika,
dodo zinatamanisha,
Ukimwi unatutisha
yailahi wangu mola,
we ndiye uliye mweza,
waja wako kutulinda,
Ukimwi unatutisha
sina mengi ya kusema,
Nisije anza sakamwa,
kwamba nawadhalilisha,
ukimwi unatutisha
Matiti Saa 6!
ReplyDeletewaafrika wameumbika jamani,Hizo mali ni orginal siyo kama za wazugu za kufoji, Mungu ibariki Afrika,
ReplyDeletepicha haiendani na makala. ungeweka matiti ya mchina ya kutengenezwa kwa madawa.
ReplyDelete