Monday, March 08, 2010

Shida Wanaopata WaBongo huko Saudi Arabia

bwana michuzi na wanablog wengine.


kwanza nawashukuru sana kwa kutoa barua yangu niliyowatumia nikiewaeleza hali halisi ya maisha huku saudia kwa sisi madereva na shida ambazo watanzania madereva na raia wa nchi nyengine tunapata. nawashukuru watz kwa kuuona ukweli ijapokuwa wapo wachache ambao kwa sababu zao walikuwa na mashaka.

napenda kueleza zaidi kuwa magenge mawili yanayosafirisha watu huko bongo wa kuwaleta huku moja linaongozwa na jamaa anaitwa bungire (jina lake kamili silijui). huyu jamaa ana wenzake wawili anaoshirikiana nao katika biashara hii. ni mtu mwenye tamaa sana ya pesa. genge hili ndilo lililonileta mimi na wenzangu huku saudia. huyu jamaa anaishi ilala na mambo mengi ya kuandikisha watu hufanya mitaani. sina hakika kama ana leseni au afisi lakini anaonekana ni mtu mwenye ushawishi mkubwa katika afisi za serikali.

wakati anatukusanya huko dar alituambia tusiwe na wasiwasi na pasi za kusafiria au viza. na kweli siku 2 tu tulipata pasi kwa kuwa wengi wetu ni mara ya kwanza kusafiri nje ya bongo. baadae akatuombea viza na tukapata ubalozi wa saudia hapo dsm. ni mtu anayeonekana maarufu au anauhusiano na wakubwa hapo dar.

genge la pili lipo mtaa wa uhuru. hawa jamaa wanaitwa madina (sijui kama ndio jina la kampuni au la mtu). hawa jmaa wamealeta wenzetu pia hapa saudia kwa kutumia njia hizohizo za ulaghai na utapeli. takriban saudia tupo madereva wengi watz tunafika zaidi ya 50 katika makampuni mbalimbali. lkn wote tumeletwa na makundi ya matapeli hao wawili. tunaendesha malori ya saruji, malori ya mafuta na magari ya mizigo mchanganyiko.

baadhi ya watu wanadhani ni chuki dhidi ya waislamu. napenda kuwaanbia kuwa madereva sote tuopo hapa saudia kutoka tz ni waislamu tena swala 5. ijapokuwa tumekusanywa dar lkn wapo wenyeji wa tanga na wengine zanzibar, lkn wengi wetu ni watu wa dar. hatuna nia ya kuwasingizia bali ndio hali halisi ya hapa na ubalozi unajua hilo. hawa jmaa hawafuati uislamu wala nini bali ni makatili na washenzi sana. hayo wanayofanya yote ni kinyume na uislamu lkn hujidai kuvaa kanzu na vilemba kama wachamungu. ni wanafiki tu.

mimi na wenzangu tulishaamua kumshtakia mungu udhalilishaji huu. hao matapeli wa dar na wenzao wasaudi wanaotunyanyasa mungu atatulipia hapa hapa duniani au kesho kiama. kama si kwa wao basi vizazi vyao vitaonja mateso kama haya tunayoyapata sisi muda huu.

lkn nimeguswa na lile tangazo na kuona kuwa kumbe hawa matapeli bado wanakusanya watz wengine na kuwaleta huku. hivyo, nawaomba watz wenzangu wasikubali kuja huku hata siku moja. bora hali ya nyumbani tz mara 100 kuliko mazingira ya huku kwa mgeni.waarabu kwao mgeni ni kama machine tu haichoki, haiumwi, haina njaa wala haipaswi kulalamika.

kwa ujumla mateso na unyanyasaji sio kwa watz tu bali pia kwa raia wengine. michuzi nakuwekea hapa hii link uone mfanyakazi wa nyumbani mkenya alivyofanyiwa hapa saudia na hii imetolewa katika gazeti la kenya. wale wanaoona kuwa saudia hawawezi kufanya mambo kama haya waone wenywe.

link yenyewe ni hii,.....

http://www.nation.co.ke/News/-/1056/840238/-/vp9oc4/-/index.html

ni mimi mtz dereva saudia...

4 comments:

  1. INAWEZA IKAWA KWELI, ILA KWELI NCHI KAMA SAUDIA ARABIA INA MAHAKAMA ZA KISHERIA NA UTAWALA WA KISHERIA UNATAMBULIKA KABISA KIMATAIFA KAMA SHERIA ZAKENI KALI KABISA KWA UNYANYASAJI,UONGO.UWIZI .NK

    MUJUE MUNGU NDIYE ANAJUWA UKWELI WA WATU HAO WANAOSEMA WANANYANYASWA.

    ReplyDelete
  2. DUH HAWA JAMAA NI WASHENZI SANA. HIVI WAKE NA DADA ZAO WANAWEZA KUEAFANYIA HIVI AU NI KWA WAAFRIKA TU?

    SERIKALI SASA IWAKAMATE HAWA JAMAA JINA NA MAKAAZI YAO WAMESHAPEWA KILICHOBAKI NI KUMKAMATA TU NA KUMFIKISHA MAHAKAMANI.

    JAMAA ANA INFLUENCE HADI UHAMIAJI... PASI YA KUSAFIRIA NI SIKU 2 TU. DUH KWELI BONGO KILA KITU KINAWEZEKANA.

    ReplyDelete
  3. hawo hawana uislamu washenzi number (1)kanzu na kamba nyeusi hawana imani hata za kibinadamu na nyiye ndo muvumilie na hii iwe funzo kwa wengine. hao ni jina tu ati waislam hawana moja la uislam

    ReplyDelete
  4. Pesa haina dini. Hao hawajali dini wanachojali ni pesa!

    ReplyDelete