Monday, May 03, 2010

Ukosefu wa Maji Safi Boston


Wadau, nikikukumbuka shida ya maji Bongo, lazima nicheke na vituko vya watu hapa Boston na miji kadhaa iliyoathirika shauri ya bomba kuu la majio kupasuka huko Weston.

Basi leo, huwezi kununua kahawa, wala chai. Sehemu chache walikuwa wanauza na walikuwa wanatumia maji ya chupa kutengeneza. Huko watu wanalia kukosa kahawa ya asubuhi, mimi nilileta kahawa ya unga kutoka nyumbani, nilichemsha maji ya kutoka kwenye bomba la jikoni kwenye microwave. Watu wamenishangaa mno! Walinitizama kama nina kichaa!

Nilienda Shaw's supermarket huko Fenway jana kununua mahitaji machache jana. Nilipoingia pale mbele walikuwa na zile packs za chupa 24 za maji, $3.99. Ilikuwa palate nzima. Nivyotoka zilibaki mbili tu!

Watu wameambiwa wasifue nguo wala kuosha nguo na hayo maji! Hapa kazini walitupiga marufuku kunawa mikono. Walisema ukinawa lazima utumie hand sanitizer.

Jana mzungu fulani kanipigia simu na kuniambia niwapigie watu wote kwenye idara yangu simu kuwaonya kuhusu maji. Nilimwambia kuwa huo bomba ulipasauka zaidi ya masaa 24 iliyopita, hivyo huenda watu wamekunywa. Na bila shaka watakuwa na habari kwa vile iliotangazwa kwenye vyombo voyte vya habari na miji kadhaa iliwapigia simu watu kuwaonya. Pia nilimwambi nilikuwa natoka kwenda kwenye shughuli saa hiyo. Mzungu alianza kulia oh watu wataugua sana usipowapigia simu! Jana ilikuwa jumapili!!!!

Hayo maji yanayotoka kwenye bomba ukitazama yanaonekana masafi kweli kweli. Huko Bongo watu wangesema ni salama. Wengine wangetia kwenye chupa na kuuza!

- Watu wamepigana mangumi madukani wakigombania chupa za maji.

- Poland Springs, Dasani, Everest, na hao wengine wanaotengeneza maji ya chupa wa ruka ruka kwa furaha. Shareholders wao watapata faida kubwa kweli mwaka huu!

- Maduka mengi yamepandisha bei ya maji. Mayor Menino anagomba!

- Watu wanafaya hoarding ya maji! Unakuwa mtu ana minivan imejaa maji! Sasa maduka wanawauzia watu crate mbili tu!

Lakini jamani, lazima niulize. Hivi watu wanashindwa kuchukua sufuria na kuchemsha maji ya kunywa? Huenda wamesahau! Maana siku hizi kila kitu ni take-out, microvae, frozen!

7 comments:

  1. Ndio maana unaambiwa Mungu yuko Afrika, nyumbani raha tupu na haugui mtu stress za mambo madogo madogo hakuna, nguo unafua kwenye maji ya kidimbwi inakauka na jua siku zinakwenda vidudu vinakufa. Wazungu hawajazoea shida, wakiletwa kule kwetu kwa mwezi mmoja tu watakao survive ni wachache sana, vyakula vya kusindikwa vinaharibu immune systems zao, bongo wanakula Organic hafi mtu!!!

    ReplyDelete
  2. Mimi ni mzungu, na wala sijasahau jinsi ya kuchemsha maji, Bwana Che Mponda. Na kwa taarifa yako, Anonymous, niliishi kwenu zaidi ya miaka mitatu, na huwa natembelea kwenu mara kwa mara, na immune system yangu bado imara. Na pia nimezoea shida mingi maisha yangu hata kushindwa kwako, kwa hiyo assumptions will get you nowhere, rafiki yangu.....

    ReplyDelete
  3. Nyie wazungu mmezoea take out na fast food. Kupika from scratch mmesahau. Wewe mzungu wa 4:20pm kama kweli mzungu basi waewe ni exception.

    ReplyDelete
  4. Bwana Anonymous ya 8:22,

    Sili take out na fast food, labda mara moja kwa mwaka. Na ninayo rafiki na ndugu zangu wengi ambawo ni hivyo hivyo. Na tunajua kupika kutoka "scratch", usiwe na wasi wasi. Nyie unalalamika kuhusu ubaguzi na stereotypes, wakati unatumia stereotypes kwa watu wengine. Kuna ile msemo ya kiswahili kuhusu "nyani haoni...", nadhani unaikumbuka.

    Mzungu ya 4:20

    ReplyDelete
  5. Hii mzungu ya 4:20 kiboko!

    ReplyDelete
  6. Jamani ni kweli wazungu wamesahau basics. Nguo zinafuliwa kwenye washing machine na kukaushwa kwenye dryer. Vyombo vinaoshwa kwenye Dishwasher. Chakula ni redimedi na taikiout. Kutembea wamesahau kila sehemu lazima waende kwa gari. Sehemu zingine kwa mwiko kutembea kwa mguu!!!! Mzungu ya 4:20 una damu nyeusi basi.

    ReplyDelete
  7. Sorry to disappoint you, lakini sina damu nyeusi, isipokuwa kama nilidanganyiwa na babu zangu (mwenye asili ya Ireland, Germany, na Italy). Shida yako ni unabaki na mawazo ya stereotypes, na huwezi kufikiria tofauti. Pole sana, ndugu yangu, tazama na macho na utajifunza mengi.

    Mzungu ya 4:20

    ReplyDelete