Hivi karibuni niliweka blog kuhusu mwananchi mwenzetu Caroline Mmary aliyepotea huko Los Angeles, California. Habari si nzuri.
Nashukuru polisi na wapelelezi huko Los Angeles wamefanya kazi. Inaelekea mume wake alimwua na kuficha mwili wa marehemu nyuma ya nyumba yao.
Mungu Ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.
Habari za kutafutwa kwa marehemu zilitangazwa kwenye TV huko Los Angeles:
http://cbs2.com/local/Missing.Woman.caroline.2.1720298.html
************************************************************
Kutoka JAMII FORUMS
Takribani mwezi mmoja uliopita kulikuwa na tangazo kwenye blogs na hapa JF kwamba kuna dada yetu mmoja alipotea na akawa anatafutwa na ndugu zake.
Taarifa iliyotolewa kwenye local TV stations za Southern California zinasema kwamba mwili wa huyo dada ulipatikana jana nyuma ya nyumba aliyokuwa akiishi. Ulikuwa umefungwa kwenye mifuko ya plastic na blanket kama takataka.
Mume wa marehemu anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo. Dada huyo alikuja kwa ajili ya kusomea kozi ya Uuguzi na alikuwa anasoma ili awe Registered Nurse. Ameacha watoto 2.
Lilian Mgonjwa alihojiwa na kituo cha TV kutoka makazi yake huko Long Beach. Kama kutakuwa na taarifa za ziada ninatumaini tutaendelea kujulishana.Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe.NB: Modes, kwa kuwa tangazo lilitolewa hapa kwenye Jukwaa la Siasa niliona ni vyema nikatoa taarifa hizo hapa na baadaye mnaweza kuihamishia popote mtakapoona inafaa kuwekwa.
Mume wake Mbongo au Mmarekani?
ReplyDeleteREST IN PEACE!
Ndugu Poleni sana inasikitisha sana jamani Kauwawa kinyama kweli yaani..
ReplyDeleteJina la bwana lihimidiwe
Mume wake ni mjerumani anaitwa Himler Schweinstigger
ReplyDeleteMh poleni sana inasikitsha sana ila ndo hvyo hakuna jinsi,mara ya kwanza niliona tangazo hili kwenye Issa Michuzi nilivyosikia bd hajapatikana nikasema ee Mungu saidi hy Mtanzania mwenzetu nduguze wamuone kumbe maskini ameshatangulia mbele za haki.Dada jamani jaribu kuangalia kwanza mm hawa watu ambao si wataifa letu naona wamekaa kimauaji zaidi, inauma sana. Mungu amlaze mahali peponi Amen. Mrs Dean
ReplyDelete