Kutoka Michuzi Blog:
Mhadhiri mstaafu wa chuo kikuu cha Dar es salaam University na mwanasiasa wa siku nyingi muda mfupi uliopita amechukua fomu za kuwania Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutimiza idadi ya wagombea kuwa 13.
Wengine ni Spika anaemaliza muda wake Mh. Samuel Sitta, Naibu Spika anayemaliza muda wake, Mama Anne Makinda, Mbunge-mteule wa Bariadi-Mashariki, Mh. Andrew Chenge, Mbunge-mteule wa Kongwa, Mh. Job Ndugai, Mbunge wa Afrika Mashariki Mama Kate Kamba, Mbunge wa Viti Maalumu Mama Anna Abdallah na Luteni Mstaafu Benedict Lukwembe.
Wengine ni Mhasibu wa Chuo Kikuu cha Saint Augustine University (SAUTI), Bw. Stephen Deya, Mjumbe wa Baraza la vijana mkoa wa Pwani Bw. Mohammed Nyundo, Kada wa CCM Bw. Kazimbaya Makwega, Kepteni Mstaafu Peter Nyalali na Mwalimu wa Shyule ya Sekondari ya Tambaza, Mwl. Salum Kungulilo.
Wishing him all the best.
ReplyDeleteEhe! Spika itamfaa! Namtakia mafanikio mema.
ReplyDeleteTunamtakia kila la kheri Dr. Aleck Che-Mponda katika harakati zake za kuwania uspika. Ni matumaini yetu ya kuwa wasomi watakuwa mstari wa mbele kupiga vita umasikini na ufisadi kwa maslahi ya watanzania wote.
ReplyDeleteDada Chemi, namfahamu mzee wako miaka mingi. Naona uspika unamfaa sana kama watakuwa fair. Usishangae lakini ukiona wanampuuza maana ndo siasa za Bongo.
ReplyDeleteKuna kazi kubwa hapo. Hiyo list hasa majina ya awali kiboko pia Old Boys network. Namtakia Mzee Chemponda best wishes.
ReplyDeleteKila la Kheri!
ReplyDeleteKazi kweli kweli! Siunajua tena bongo yetu, mzuri anayefaa ni yule 'mwenzetu' ili alinde masilahi `yetu' kwa manufaa `yetu' na watoto 'wetu'. Kama sio mwenzetu hata kama unafaa, utabigwa kikumbo kama hujulikani na hata kutungiwa wimbo wa uwongo kuwa `sio mzawa, au mbongo'
ReplyDeleteTWAMTAKIA KILA-LAHERI KWANI AKISHINDA NI KWA MANUFAA YA TAIFA KWA UJUMLA!
Akishinda itakuwa vizuri sana kwa taifa. Best wishes.
ReplyDeletenakumbuka alishawahi kuwania tena akapata kura moja, nadhani ilikuwa ya kwake tu. Nadhani kwa sasa atakuwa amejipanga.
ReplyDeleteChama cha mafisadi kimeshatoa majina 3 ya wanawake tupu Anna Makinda, Cate Kamba Na Anna Msekwa mke wa spika wa zamani.
ReplyDeleteAtawaweza mafisadi?? au naye anataka ajiunge nao?
ReplyDelete