Mwaka 1990 kuna dada fulani (Marehemu) huko Manzese aliyetengeneza maforonya na mashuka ya vitenge. Watu walimcheka.
Leo wazungu wanatengeneza makochi ambayo yamefunikwa (upholstery) na vitenge. Tena wanaziuza bei mbaya. Hebu cheki hizo kochi pichani, moja dola $1,700! Hizo ottoman za kuwekea miguu dola $200! Acheni kudharua vitenge na khanga zetu. Tengenezeni maseti ya mashuka na maforonya mpate kibunda....ohhooooo! Exported from Tanzania!
Mnaweza kuona bidhaa zaidi kwa kubfoya hapa: ANTHROPOLGIE.COM
Hii bab kubwa, manake tunajitangaza, mfano kwenye hayo makochi wanaweka misemo ya kiswahili, mfano
ReplyDelete`hata ukinikalia hutanikumbuka...'
Changamkeni wabongo. Kumbe miaka yote hii tungekuwa tuntajrika kwa kuexporti makochi ya vitenge!
ReplyDeleteUchumi tunao tumeukalia tu, utashangaa Wakenya watakavyochangamkia hiyo biashara. Siku moja nimeingia duka la HMS UK mwaka 2007 nikakuta gauni ya summer imeshonwa kwa kanga nzito ya urafiki, lakini limetoka Kenya!
ReplyDeleteKazi kubwa tunayoijua ni kulalamika tuu!
Sisi tunadharau wenzetu wanaona njia ya kutengeneza mapesa!
ReplyDelete