Wednesday, December 15, 2010

Rest in Peace Dr. Remmy Ongalla

Baadhi ya walombolezaji nje ya nyumba ya Dr. Remmy Sinza
Mama Yangu mzazi Rita Che-Mponda akimpa pole Mama Ongalla

Kali Ongalla akicheza na kasuku wao

Mjane wa Dr. Remmy, Toni Ongalla, wanae Tom na Kali masaa machache kabla Dr. Remmy kufariki dunia.


Wadau, siku ya jumapili 12/12/10, nilialikwa nyumbani kwa Dr. Remmy na mke wake Toni. Tunafahamiana na famila ya Ongalla tangu mwaka 1978. Hivi karibuni walikuwa wamehamia kwa muda nyumba huko maeneo ya Africana kwa vile nyumba ya Sinza inakarabatiwa.

Basi, nilifika huko kwenye saa 7 na nusu. Toni alinipeleka chumabni kumsalimia Dr. Remmy. Dr. Remmy alikuwa amelala kwenye kitanda na mwanae Tom. Mke wake alisema, "Chemi amekuja kukusalimia, unamkumbuka Chemi?"

Dr. Remmy aliwaambia anataka kwenda sebuleni kukaa. Walivyotoka kwenda kumchukua kiti cha kumsukuma kwenda huko (walikuwa wanatumia viwili vya palstiki kwa vile hawakuwa na wheelchair, Dr. Remmy aliinuka mwenyewe kitandani na nguvu zake. Alikaa akanitazama sana, ila hakusema kitu. Nilimwambia pole kwa kuumwa lakini atapata nafuu. Walileta kiti halafu walimpeleka sebuleni kwenye meza ya kulia chakula.

Chakula kililetwa na nilikula na familia huko natazamana na Dr. Remmy. Mara kadhaa alishika mke wake mkono kama vile anamwambia asiwe na wasiwasi mambo yote yatakuwa sawa. Dr. Remmy hakuweza kula lakini alikunywa soda kidogo na supu. Wanae Kali na Tom walimsihi baba yao ale chakula ili apate nguvu. Baada ya muda aliomba arudishwe chumbani, wanae walimpeleka.

Mimi na Toni tuliongea sana maana Dr. Remmy alikuwa na matatizo ya mafigo na marehemu mume wangu Rev. Whitlow alifariki kutokana na maradhi ya figo. Toni alisema kuwa Dr. Remmy alipata Stroke (kiharusi) tangu mwaka 2000. Toni aliniuliza kama ingekuwa vizuri awaite wanae walio nje kuja kumwona baba yao. Nikamshauri awaiite mara moja, maana niliona hali ya Dr. Remmy ilikuwa ya kutisha, lakini sikutegemea kama angefariki siku ile. Alikuwa bado ana mwili. Tuliaagana na familia ya Ongalla, halafu nilienda zangu.

Kesho yake nilitoka Muhimbili baba yangu alikolazwa kwenye saa nne na nusu kwenda kupanda daladala kwenda Kariakoo kwenye stendi pale Muhimbili. Nikiwa nimekaa kwenye basi walitangaza kwwenye redio kuwa Dr. Remmy amefariki dunia. Nilianza kupiga mayowe na kushgangaa kuwa mtu niliyemwona akiwa haia masaa machache kabla alikuwa amefariki. Si watu walinizunguka kusikia kuhusu ile last supper na Dr. Remmy.
Sikumpiga picha maana ningependa ktumukumbuke kama alivyokuwa. Mungu awape familia nguvu katika kipindi hiki kigumu.
REST IN PEACE DR. REMMY!

5 comments:

  1. Ikiwa siku yako ya kifo utaondoka tu! Apumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  2. Duh, kweli wewe ulibahatika kwenda kumwanga akiwa hai...Hiyo ndio njia yetu, mungu amlaze mahala pema peponi!

    ReplyDelete
  3. Pole sana Chemi,japo pia ni bahati ya pekee kuweza kuagana naye kabla ya umauti kumkuta. Rest In Peace Dr. Remmy.

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  5. Haya maelezo ya dakika za mwisho mwisho juu ya Dk Remmy Ongala ( Rama Zani Mtoro Ongala, jina la kuzaliwa) yamekita ndani kwa hisia na utulivu wa kuhuzunisha na kufurahisha.

    ReplyDelete