Saturday, January 15, 2011

Clip From Maangamizi the Ancient One



Hii ni clip ktuoka sinema Maangamizi the Ancient One. Ni sinema ya kwanza ambayo Tanzania ilietua katika Academy Awards (Foreign language category). Ingawa haikuchaguliwa kuwa katika sinema tano bora za mwaka huo 2000 ilikuwa hatua kubwa sana kwa Tanzania kujulikana katika dunia ya sinema.

Je, sinema gani kutoka Tanzania itakuwa ya pili kutueliwa? Kwa wasiojua mimi niliigiza kama Nesi Malika katika Maangamizi, ilikuwa sinema yangu ya kwanza. Ilipigwa Bagamoyo mwaka 1994 kabla mji haujajengwa kama ilivyo sasa.

4 comments:

  1. Nilipata kuiona filamu hiyo na ni jambo la kufurahisha kwamba inaakisi hali halisi na utamaduni wa Watanzania. Hizi filamu za sasa za Tanzania zinasikitisha. Tunachokiona ni majumba na magari ya kifahari tu. Nadhani hata wewe Chemi huwa unapata nakala huko Marekani na unaweza kutoa tathmini yako. Hawa jamaa wakikosolewa hukimbilia kudai kuwa wanaonewa wivu.

    ReplyDelete
  2. Anonymous wa 6:41am, asante kwa comments zako. Umesema kweli mara nyingi tukisema kitu ni kweli tunaambiwa tuna wivu. Mfano niliona mwimbaji maarufu wa Bongo akiimba hapa Marekani. Nilipendekeza vitu fulani ili aweze kuonyesha umaarufu wake zaidi na kuonekana kama professional. Loh, kosa! Wacha nishambuliwe mpaka matusi ya nguoni. Jamani, si kukosoa ni funzo. Watu wawe wazi kujifunza.

    ReplyDelete
  3. chemi umesema kweli.

    ReplyDelete
  4. Pole sana Da Chemi lakini ndivyo wasanii wetu wa Tanzania, hasa hawa wa sasa, walivyo. Wale waliowahi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania ndio kabisaaa hawashikiki. Wanajiona wamemaliza kila kitu na hakuna yeyote anayeweza kuwaambia chochote.

    ReplyDelete