Enzi zetu unalazimishwa kununua Ice Krimu na Maandazi za Mwalimu. Sasa unalazimishwa kutumia internet na scanner ya shule!
*********************************************
Nimepata hii kwenye email:
Nina mtoto ambaye anatarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka
huu kama mtahiniwa wa kujitegemea,
Shuleni kwao waliambiwa kuwa form hawana kwa kuwa baraza la mitihani
limebadilisha mfumo wao wa utowaji hizo form, hivyo wanalazimika
kuingia kwenye mtandao wa necta{website) na kujisajili kwa ku-upload
picha zao na kuingiza baadhi maelezo yao na hatimaye kupata form
ambayo wanatakiwa kuiprint na kwenda kulipia...
Nime mfanyia wanangu hayo yote na kumpa hiyo form kwaajili ya kwenda
kuwekwa sahihi na muhuri shuleni kwao.
Na baada ya kuipeleka jana waliambiwa wakazichukue leo...
Cha kushangaza ni kwamba uongozi shule ya Makongo, ameingia darasani
kwao na kuwa hoji ni wanafunzi wa ngapi wameji andikisha necta, karibu
wanafunzi wote walikuwa wamejisajili kasoro wa nne tu ndio walikuwa
hawajajisajili.
Baada ya kugundua wanafunzi wengi wamekwisha jisajili, bw. Maebe
aliwaambia kuwa usajili wao ni batili, hivyo wanapaswa kujisajili tena
hapo shuleni...
Baada ya kumuhoji mwanangu nime gundua kuwa..
Mwanzo uongozi wa shule ndio uliowataka wakajisajili kwenye ma-
internet cafe, kwa kuwa wao scaner na printer zao zilikuwa kuwa mbovu,
sasa baada ya kununua nyingine ndio wameona bora kuwadanganya
wanafunzi kuwa kuna taarifa wamezipata kuwa kuna uwezekano wa baadhi
yao kushindwa kufanya mtihani eti kwa kuwa inawezekana hawakujisajili
vizuri..
Hivyo watawasajili tena kwa kutumia internet ya shule na printer zao
kwa gharama ya tsh elfu 5,000.
Huu ni wizi wa hali ya juu jamani, tunapaswa kuukemea kwa nguvu
zote...
No comments:
Post a Comment