Tuesday, March 15, 2011

Isaidie Sinema ya Weusi - Picture Me Blue No More

Lazima niwasifu hao weusi wa Atlanta. Wanataka kutengeneza sinema ambayo naona itakuwa nzuri kuliko Precious.

Wanafanya kampeni wenyewe ili kupata pesa za kuitengeneza. Ukitaka kuchangia unaweza. Mchango unaanza kwa dola $5 tu!

Niliwasiliana nao, nikawaambia kwa nini wasimwombe Oprah awasaidie. Walisema wamemtumia ujumbe mara nyingi lakini hawapati majibu. Hata ile sinema ya Precious ilikuwa hivyo hivyo ila ilipopata huko Sundance Film Festival maarufu Oprah na Tyler Perry walikuwa mstari wa mbele kuisukuma.

Mwaka huu kulikuwa hakuna sinema ya weusi wala waigizaji weusi waliyofanikiwa kuingia katika mashindano ya Oscars. Perla Fay Humphrey na kampuni yake OnyxPearl wakifanikiwa kutengeza hii sinema huenda mwaka 2013 ndo itakuwa sinema ya weusi inayoongoza.

Natumaini watafanikiwa na lazima niseme ni mara chache kuona waMarekani weusi wenye moyo wa kufanikiwa kutengeneza sinema ya hali ya juu kama hii. Mungu yu mwema watafanikiwa.
Nilisikia habari za mpango wa kutengeza hii sinema mwaka jana Agosti walipokuwa na Casting Call kutafuta waigizaji. Ubaya ilikuwa Atlanta na Los Angeles hivyo nilishindwa kwenda. Kuna kikundi ha waigizaji weusi kutoka hapa Boston ambao walisoma vipande vya script na wali-blow kwa ilivyo nzuri.

Sinema Picture Me Blue No More itahusu maisha ya mtoto wa kike maskini huko Georgia ambaye anafanikiwa kwenda Chuo Kikuu na kuwa na maisha bora ingawa aliishi katika dhiki, uonevu, kubakwa nk.

Mnaweza kupata habari za kampeni yao HAPA:

http://www.onyxpearl.com/picturemebluenomore/

No comments:

Post a Comment