Monday, May 02, 2011

Osama bin Laden Ameuawa!



Jana usiku nilikuwa nashangaa kwa nini majirani zangu wanapiga makelele za kushangilia sijui nini usiku wa manani. Leo asubuhi kuamka ndo nasikia kwenye taarifa ya habari kuwa wanajeshi wa Marekani wamefanikiwa kumwua Osama bin Laden huko Pakistan. Serikali ya Marekani ilijitolea kusafirisha maiti ya bin Laden kwao Saudi Arabia kuzikwa, lakini serikali ya Saudia walisema hawataipokea. Hivyo, maiti yake ilizikwa baharini kusudi watu wasipate nafasi ya kumwabudu.

Osama bin Laden alisababisha vifo vya maelfu ya watu. Atakumbukwa zaidi kwa maafa ya 9/11 mjini New York, lakini tusisahau kuwa kaua waTanzania na waKenya mwaka 1998. Tanzania na Kenya tulimkosea nini bin Laden?

Habari za kifo cha bin Laden ni habari njema. Ila tusisahau kuwa kuna wengi ambao watataka kumwiga na kuendelea kumwaga damu ya watu wasio na hatia.

6 comments:

  1. Duuh! Wapo wengi hawo, wakati nasoma hii, jamaa mmoja alikuwa akituhadithia lile bomu la Hiroshima, ...jamani dunia hii amani itakuja lini, tuache haya...kuuana, visasi , chuki!

    ReplyDelete
  2. Isomeke Obama Bin Laden badala ya Osama Bin Laden.

    ReplyDelete
  3. Da Chemi hiyo tittle ndo ulivymaanisha au vidole vilipata kwikwi?

    ReplyDelete
  4. Wadau naomba samahani! Nimerekebisha. Nilikuwa nimesafiri jana kwenda kwenye msiba wa rafiki hivyo sikuwa na access ya computer.

    ReplyDelete
  5. Ding, Dong Osama's dead! Bado Gaddafi!

    ReplyDelete
  6. DAILY PRAYER TO OBAMA

    we genuflect barack holy black jesus

    born of biracial love in honolulu

    worshiped by democrat masses

    save us from the palin devil

    perform miracle Gabby Giffords recovery

    give us our daily healthcare bread

    open red sea of immigrant borders

    free us from corporate slavery

    cast out wall street money changers

    end republican global war crusades

    save mother earth climate change

    perform miracles of green technology

    on your cross of tea party torture

    bless you for eight years

    Your prayer should be directed to the Navy Seals, they risked their lives to kill him, not your beloved Obama.
    ...

    ReplyDelete