Tuesday, May 31, 2011

Wanafunzi wa Tosamaganga Wapigwa Mabomu ya Machozi - Mwandishi wa Habari Atiwa Mbaroni!


(Pichani wanafunzi wa shule ya sekondari chini ya ulinzi wa FFU kabla ya kupigwa mabomu ya machozi. Picha na Franci Godwin)
Wadau, kumradhi kwa kuchelewa kubandika habari hizi. Nilikuwa na matatizo ya kompyuta.

Habari kutoka Iringa zinasema kuwa Mwandishi wa Habari Francis Godwin ametiwa jela baada ya kuripoti kuhusu mgomo wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tosamaganga na hatimaye kupigwa mabomu ya machozi ya FFU.

Nabandika habari alizoandika Kaka Francis. Kwa Picha na Habari zaidi BOFYA HAPA:

May 31, 2011

BREAKINGNEWS.....NIPO CHINI YA ULINZI WA POLISI YATOSA YAMENIPONZA

Mwandishi wa mtandao huu Bw Francis Godwin kwa sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi baada ya kukamatwa katika shule ya sekondari Tosa maganga akifuatilia sakata la mgomo wa wanafunzi
***************************************************
May 30, 2011

Hali ya usalama si shwari katika shule ya sekondari Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivi sasa wanafunzi zaidi ya 1000 wapo porini wakikimbizwa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ambao wanatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa katika maandamano ya amani kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuulalamikia uongozi wa shule hiyo.

Hadi hivi saa mabomu zaidi ya 10 ya machozi yamepigwa kuwatawanya wanafunzi hao ambao baadhi yao wanadaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na miti wakati wakikimbia porini kukwepa mabomu hayo huku wananchi wa Mseke wakikimbia nyumba zao.

Polisi wamewazuia waandishi wa habari akiwemo mmiliki wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao waliokuwepo eneo hilo wakifuatilia tukio hilo kuendelea kuchukua habari hiyo .

Undani wa habari hii ya picha zaidi zitakujia hivi punde japo kwa sasa binafsi macho yanauma sana kutokana na moshi ya mabomu hayo kunikuta pamoja na mwanahabari mwenzangu wa Radio Ebony Fm japo

*****************************************************
May 30, 2011

Hari si shwari shule ya sekondari Tosamaganga Iringa wanafunzi wote zaidi ya 1000 wameandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa Iringa kupinga madai mbali mbali sasa wanaingi barabara kuu upo uwezekona wa mabasi kuzuiwa FFU Watanda shuleni habari kamili na picha zinakuja!

**********************************************************

3 comments:

  1. Tanzania tunaelekea wapi? Wanafunzi wanapigwa na mabomu ya machozi! Kwanza UDSM sasa Tosamaganga!

    ReplyDelete
  2. Jamani polisi wa CCM si wanafundishwa kuwatia adabu waipingao serikali yao?
    natamani siku moja wabunge waamue kuandamana hata siku moja nione polisi watafanya nini.
    hata waandamane kwa bahati mbaya tu, wajifanye hamnazo dhidi ya serikali.

    ReplyDelete
  3. My dear wabunge waupinzani walitaka kuandamana nafikiri uliona matokeo yake. tatizo kubwa la tanzania hatutaki feedback. kiongozi yeyote asiyepokea feedback anamatatizo. na hii ndiyo nchi yetu.kiongozi hata kama amechemsha anataka kusifiwa tutafika wapi? hawataki mtu yeyote mwenye fikra pevu (critical mind) na ndo sababu wanaanza kuwadhibiti vijana. Hawajui kizazi hiki siyo cha ndio mzee au ndio mwalimu? kizazi hiki ni cha mwalimu sijaelewa, sikubaliani nawewe eleza zaidi.

    ReplyDelete