Tuesday, November 08, 2011

Joe Frazier Afariki Dunia!

Joe Frazier (kushoto) na Muhammad Ali



Joe Frazier (1944 - 2011)

Bondia maarufu   Joe Frazier amefarikia dunia.  Frazier alipigana na Muhammad Ali mwaka 1971 katika pambano kali iliyoitwa 'Fight of the Century'.  Habari zinasema kuwa madaktari waligundua kuwa Frazier anaumwa kansa ya ini wiki sita tu zilizopita.  Alikuwa ana miaka 67.   Frazier hakumpenda Ali kwa sababu alijaribu kumsaidia alipopatwa na matatizo ya kuzuiliwa kupigana. Jibu la Ali ilikuwa kumwita Frazier 'Sokwe' (gorilla) kwa vile alikuwa mweusi sana kulingana na weupe wa Ali. Mungu ampumzishe mahala pema mbinguni. Amen

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

8 comments:

  1. FRAIZER has never fought in ZAIRE

    ReplyDelete
  2. Yes, that's true, my bad. The Rumble in the Jungle was Ali Vs. George Foreman.

    ReplyDelete
  3. Toeni upumbavu wenu hapa, Ali hakumwita Frazier Gorilla kwa sababu ya weusi, Ali alimwita Frazier Gorilla kwasababu Frazier alikuwa anakubali kushikiwa akili na wazungu, kutumiwa na wazungu, na alikubali kuwa "white hope" wakati anapigana na Ali. Kwa ushahidi, wakati wa pambano lao la 1971 madison square garden, wazungu wote pamoja na John Louis(another uncle tom of his days) walikuwa wanamshangilia Frazier; wakati wamarekani weusi wote walikuwa wanamshangilia Ali.

    Baada ya Ali kuwa muislamu na kubadilisha jina, wazungu walimtumia Frazier na Frazier akakubali kutumiwa na wazungu kwamba hawezi kumtambua Ali kwa jina lake jipya. Frazier akaendelea kumwita Ali "cassius clay" jina la kitumwa ambalo Ali alikuwa halitaki. Ndipo Ali akaja kusema; "Gorilla hili linatumiwa tuu na wazungu".

    Ali alimwita Floyd Patterson "Rabbit"; na alimwita George Foreman "another sony liston";

    Ali aliwaita mabondia wengi tuu majina tofauti na kwa sababu tofauti.

    Halafu wewe chemi ni mwandishi wewe; tunajua kwamba hili siyo gazeti, lakini kama mwandishi angalau uwe unakuwa "professional" angalau kidogo kwa kuandika vitu unavyovijua kulikoni kukurupuka namna hii.

    ReplyDelete
  4. Nawe Matangalu si siri kuwa Ali alikuwa anaringa kuwa yeye ni Handsome na Frazier ana sura mbaya na anafanana na sokwe. Hayo mengine yalisemwa ili ali asionekane ana roho mbaya. Ni kweli Frazier alijaribu kumsaidia wakati alipata matatizo halafu Ali alizaba kibao. Hakuwa na shukurani hata kidogo. Ndo maana sasa Ali anaumwa na hajiwezi hajatubu madhambi yake bado.

    ReplyDelete
  5. Ali aliwahi kusema "Im more handsome than anyone in Hollywood, and Im black". Sikumbuki kwamba Frazier amewahi kuwa "in hollywood".

    Kama "ujinga wa kiroho" ndiyo unaokusumbua na kudhania kwamba Ali anaumwa kwa sababu ya madhambi , Frazier amefariki kwa maradhi vile vile akiwa na miaka 67. Ali bado anaishi na ana miaka 69.
    Mimi kama mwanadamu, Mungu hakunipa uwezo wa kupima madhambi ya mwanadamu mwengine, na imani yangu inanikataza kujipa kazi isiyonihusu kama hiyo.

    Msiandike upumbavu humu kwa sababu hizi blogs zinasomwa na watoto wadogo.

    ReplyDelete
  6. Mmh Dada Chemi unaandika kiudakuudaku kweli... yaani hiyo umeiweka hapo kuchocheachochea tu.
    Wengine ndio wameshaiingia kwenye mtego wa kuwa divided and ruled...

    ReplyDelete
  7. Matangalu: maneno haya Upumbavu, ujinga si ya mtu mstaarabu kama wewe. Ume spoil hata mchango wako mzuri. Matusi hayaelimishi!

    ReplyDelete
  8. R.I.P. George Foreman. It's true Ali thought he was all that good looking and ridiculed his opponents! Where is Ali now? I bet he wishes he had been more civilized.

    ReplyDelete