Saturday, December 10, 2011

Taifa limefikia Pabaya kwa Ugonjwa wa Udini


Naomba kulitumia jamvi hili kuelezea hisia zangu na uchungu nilio nao kwa taifa hili kwa jinsi mbegu ya udini ilivyopandwa na kutishia uhai wa nchi yangu niipendayo sana ya Tanzania. Labda nianze kwa kusema kwamba binadamu wote tumezaliwa ama kuumbwa na sura ya mfano wa Mungu lakini sisi tumeongeza sura za ziada juu ya wanadamu wenzetu. Matokeo yake ni kwamba mbali na sisi sote kuumbwa na Mungu mmoja na wote kuwa sawa mbele zake, kwa bahati mbaya dini tulizo nazo zimetufanya tuweke sura za ziada kwa wanadamu wenzetu na kuwahukumu na kuwachukia kwa vigezo vya dini zetu na kwa bahati mbaya sijawahi kusikia kuwa katika hizi dini zetu kuna vyeti maalumu toka kwa Mungu vinavyotuambia dini zetu ni bora kuliko nyingine na hivyo zina haki ya kuhukumu wengine. Ni viongozi wetu wa dini ndio wanaotulisha chuki dhidi ya wengine na sisi tunayapokea mafundisho yao bila kuhoji.

Hebu niende kwenye hoja yangu ya leo. Nimesoma Mwananchi leo kuwa Shule ya sekondari ya Ndanda imefungwa kwasababu ya mgomo baridi wa wanafunzi wa kiislamu wanaodai kuwa wanabaguliwa, wanataka udahili ulio sawa kati ya wakristo na waislamu na wanataka wajengewe msikiti hapo shuleni. Habari hii imenikumbusha vuguvugu hili ambalo limeibuka sana tangu wakati wa uchaguzi mwaka jana na vuguvugu hili la waumini wa kiislamu limekuwa likichochewa pia na magazeti ya kiislamu, vyuo na shule za kiislamu na kwa upande wa dini ya kikristo nako lipo vuguvugu la kuwaambia waumini wao wajipange dhidi ya wenzao.

Yapo matukio kadhaa yaliyotokea nchini ambayo yanaashiria kukua kwa chuki hizi za kidini nchini. Nikikumbuka machache, ni nyaraka za kidini wakati wa uchaguzi hususani zile za kuwahimiza waislamu kutomchagua mkristo, kauli mbiu za vyombo vya habari vya kidini kuwahimiza waumini wao kupambana na mfumo kristo nchini, vurugu za kidini chuo kikuu cha Dodoma, mihadhara ya kidini huko Arusha na vurugu za kidini huko Mwanza nk. Inasikitisha sana kuona sisi watanzania wa leo tunafanywa maadui kwa njia ya dini za kigeni. Naionea huruma Tanzania yangu inakoenda si kuzuri.

Kamwe sitasita kupaaza kilio changu kuwalaumu wanaisasa wanaotumia dini kwa maslahi ya matumbo yao na si taifa hili. Nakilaumu chama cha mapinduzi, tena nakilaumu kwa wazi kabisa kwa kubeba bango la udini kama mtaji wa kisiasa na kuliacha taifa likichakaa. Taifa lililosimikwa katika misingi ya uzalendo leo linasimikwa katika misingi ya ubaguzi. Ninashindwa kuelewa kwanini ndugu zangu waislamu wanawaona wakristo kama maadui hapa nchini na siku zote wameaminishwa hivyo, kwanini?

Nataka tujiulize kwa uwazi kabisa, hivi ni wakristo waliowazuia Zanzibar kusiwe na shule na vyuo? Hivi ni wakristo wamewazuia kujenga vyuo au kukosa pesa za kusimamia misikiti na taasisi zao? Hivi ni wakristo ndo wanaoenda kwenye shule kuwaachisha watoto wao masomo? Hivi ni wakristo ndio wanaoandika majibu ya watoto wao kwenye mitihani? Hivi ni wakristo ndo wanaowatuma wawe na migogoro kwenye misikiti? Mbona hata wakristo wanayo migogoro yao na wanaimaliza? Hivi, nataka kujua, hawa wakristu ndo wanaowazuia wao kuswali? Wakristo wanaingiaje kwenye mfumo wa maadili kwenye misikiti na madrasa ya waislamu? Hivi watanzania tumefikia katika hali ya kuchukiana kiasi hiki kwa misingi ya dini zisizo zetu?

Kama kuna jambo ambalo sitasita kulisema wazi ni hili la CCM kutumia dini kama mtaji wa siasa kila kinapofika kipindi cha uchaguzi. Lakini chuki zilizojengwa sasa ni hatari zaidi na ninasikitika kuwa taifa litaangamia. Najiuliza, mwaka jana walidai Chadema ni chama cha kidini, lakini sijawahi kumwona wala kumsikia mgombea wa Chadema wa urais akitumia makanisa kwa kampeni. Hakuwahi kuomba achangishe harambee za makanisa, sherehe za kidini nk, lakini hawa viongozi wa CCM wanatumia makanisa na misikiti kujinadi. Nani mdini hapa? Naipenda Tanzania, nalipenda taifa langu, nawachukia sana wanaoligawa taifa hili kwa misingi ya ukabila, udini na rangi. Sote tuungane kulitetea taifa letu.

Asanteni sana kwa kusoma waraka wangu huu mrefu.
Mdau FK

8 comments:

  1. We mwenyewe MDINI, au definition yako ya UDINI ni pale muislam anapodai haki yake tu?

    Ovyoo, maana unachokifanya nikuwalaumu waislam na kutetea ukristo, kisha unalalamika eti watu waache udini! We huo wako ni nini? Yaani unavyowachukia waislam na uislam mpaka unaumia rohoni! Na bado sasa waislam wameamka, watadai haki zao walizonyang'anywa na Mkatoliki mwenzio JK Nyerere...hakuna kulala, tutawabana kila kona! Hii nchi yetu sote, tutagawana uongozi kwa usawa, tutagawana rasilimali kwa usawa, na mkituletea zakuleta mtatafuta sayari ya kwenda kuishi!

    "SISI MUJAHIDYNA TUNAPENDA KUFA, KULIKO KUISHI HUKU TUKIDHULUMIWA" wapelekee ujumbe huu makafiri wenzio!

    ReplyDelete
  2. Kama kweli huyo mwandishi wa gazeti la Mwananchi hajatia chumvi kuna tatizo kubwa TZ. Hayo madai ya wanafunzi wa kiislamu wanaodai kuwa wanabaguliwa na wanataka udahili ulio sawa kati ya wakristo na waislamu nakujengewe msikiti hapo shuleni nijambo la ajabu kabisa. Huwezi kutegemewa mtu makini hata kuliibua jambo kama hilo katika jamii ya watu waliostaarabika maana niaibu kubwa. Inasikitisha sana.

    Bila shaka hapo ndanda kuna misikiti mingi tu nahao vijana hawaendagi KUSWALI. Binafsi naona hilo dai lao ni dalili za kuleta vita na magomvi yenye mlengo wa kidini kwa wale watakao pinga ombi lao.

    Jamani ebu tukae kitako na tujiulize! hivi kweli tukianza kudahili vijana wetu kwa kutumia creterion ya dini na sio performance tutafika??? Nielimu ipi tutakayoijenga hapa Tanzania!!.

    Kwangu naona nibusara kumjudge mtu kwakigezo cha content alionayo kichwani (composition yake kichwani) na sio kwakigezo cha udini. Angalau wangesema hiyo shule haina wataoto wakutosha wakike, tungeelewa kuwa wanataka kuwainua dada zetu lakini dini hapana jamani.

    Au wanataka kutuambia kua performance ya mtu darasani inakuainfluenced na dini yake? labda wamefanya utafiti watuletee majawabu hapa.

    Performance= f (Aina ya dini).

    So ukiwa mwisilamu unafeli na ukiwa mkiristo automatically unafaulu. So kuleta usawa wa elimu tuhakikishe kuwa tunadahili sawakwasawa waisilamu na wakristo. Lakini kama mathematical relatioship ndio hiyo watakua wanajichuja wenyewe huko ngazi za juu, labda iwe katika kila level ya elimu.'o' Level, Advance Secondary, College, Universities, Masters, PhD na makazini. Looh kazikwelikweli patakua hapatoshi. Sijui hii inaapply katika dunia ipi?

    Nawaasa hao vijana watambue kua hii dunia niyaushindani 'natural selection'. Nahakuna shaka waliobahatika kusoma mpaka chuo kikuu pale UDSM tumeshuhudoia kuwepo kwa wahadhiri makini kabisa waisilamu siamini kama kunamtu amewabeba, wanafanya kazi nzuri na wanaheshimika sana. Nasifa yao kubwa huwezi kuwasikia wanaongelea dini zao na wanashirikiana vizuri tu na wanataaluma wa dini zingine. Mfano ni professor Juma wa fuculty of Law.

    Kwakweli mambo haya siyakufumbia macho. Hao vijana wasome kwabidii watachaguliwa tu nasio kutafuta huruma ya dini zao.

    ReplyDelete
  3. Mie ni Mtanzania wa asili ya Kihindi baba yangu babu yangu wote
    wamezaliwa Tanzania kule Mwanza naongea kisukuma kama sina sina akili
    nzuri miaka michache iliyopita niliondoka nchini kwa ajili ya masomo
    nje ya nchi hali ilikua tofauti sana na sasa naeleza kidogo .

    Sikuhiyo nipo mjini pembeni ya hoteli ya kilebanoni pembeni ya msikiti
    round about nikaulizia ofisi ya kupanga pale waliponiona tu nikapewa
    habari eti hawakodishi wahindi lile jengo la wazawa tu nilivyodadisi
    nikagundua jengo ni la mheshimiwa Fulani aliwahi kua waziri wa
    biashara na viwanda simba iddi hope you know him na ile kauli mbiu
    yake ya UZAWA .

    Nimegusa eneo moja kati ya mengi yanayoikabili nchi hii kwa miaka
    nenda rudi hata hivyo sikati tamaa vikundi vya watu hawa tuwaanike
    jamii iwajue kwa ubaguzi wao .

    Babu yangu alivyostaafu kazi yake Tanzania alienda kupumzika India kwa
    ndugu wengine huko aliumwa sana akamwambia mtoto wake yaani baba yangu
    anataka kurudi kwao Mwanza na hiyo ilikua safari yake ya mwisho maana
    alifariki akisisitiza azikwe hapo mkoani .

    Huu ubaguzi unaoendelea kukua hapa Tanzania sio mzuri kwa maisha yetu
    watanzania kwa sababu wanaoathirika sio wa dini moja linaloathirika ni
    taifa ambalo halina dini na hata makundi ya jamii yasiyona dini au
    dini tofauti hata rangi tofauti .

    Kumbukeni wakati wa uchaguzi Dr A Rukoma amekimbia jukwaa hili aliwahi
    kutamka eti kikwete ndio raisi wa mwisho muisilamu mkauchuna

    CHONDE CHONDE .

    ReplyDelete
  4. Mimi naona umefika wakati tuache kulaumiana na hata kunyoshea vidole
    makundi mengine ya kijamii kwa matatizo yanayoendelea nchini haswa
    yaliyonyeti kama haya ya udini yanayogusa ubinafsi wa mtu na utu wake
    kwa ujumla maana kila mtu anahisia zake na anaweza kuchukuwa uamuzi wa
    kuathiri pande zote za yule anayelaumu na kunyoosha vidole na hata
    yule anayelaumiwa .

    Kwanini usiwe kama Afrika Kusini ambapo kulikuwa na kamati za
    upatanishi na maridhiano ? hapa kwetu inashindikana nini ? ndio kuna
    jamii zimekuwa zikilalamika miaka yote 50 ya uhuru wa nchi yetu na
    malalamiko hayo yamehamia kwenye vizazi na kugeuka uadui kati ya jamii
    na matabaka mbalimbali , njia bora na kuwa na kamati za maridhiano
    kama ilivyokuwa afrika kusini watu wakasamehana na kujenga nchi yao ,
    kama ilivyokuwa Rwanda watu wakasameheana – tusikubali suala hili
    likuwe mpaka watu waumizane tuanze kupelekana kwenye mahakama za
    kimataifa kama Jirani yetu Kenya hiyo haitolea upatanisho nchini .

    Tuache kulalamika tufanye kazi , tumekuwa tunalalamika kwa miaka 50
    yote bila kufanya chochote na wanaoongoza kwa kulalamika bila kuja na suluhisho ni sisi wasomi tunaotakiwa kuwa chachu ya mabadiliko na maelewano katika jamii .

    ReplyDelete
  5. Aliyeuanzisha udini keshakufa, sasa katuachia matatizo sisi.

    Na huyo Dr. A Rukoma kama ni kweli amesema kwamba eti Kikwete ndiyo rais wa mwisho muislamu aendelee kufikiria hivyo tuu. Sisi waswahili twasema "ajidhaniaye amesimama......". Kama hii ikulu wataibeba na kuipeleka huko kwao wanapotoka, labda ni kweli Kikwete ndiye rais wa mwisho muislamu. Lakini kama ikulu ipo hapa kwetu sisi, basi mkae mkielewa kwamba tunao uwezo wa kuamua kwamba mkiristo hata mmoja asiwepo Dar-es-salama.
    Siku tutakapoamua kuziba barabara ya morogoro kuanzia kibaha maili moja, na bara za kwenda pwani zitazibwa kisarawe na mkulanga; basi kama wewe ni kafiri na upo ndani ya "perimeter fence"; hapo ndipo utakapovuta pumzi zako za mwisho.

    ReplyDelete
  6. well said sister, udini upo wakati huu zamani nikiwa shule tulishirikiana na kila mtu na kuheshimu taratibu za dini nyingine tukatembeleana makanisani na misikitini wakati wa sherehe, sasa hivi taabu, udini umeshamiri sababu umeshazisema dada

    ReplyDelete
  7. katika maoni yote humu wenye udini ni wanaowaita wenzao kafiri.kaeni na uduni wa mawazo na elimu duni hiyo ndiyo saizi yenu.anzisha hayo mnayoyataka,funga barabara kama ulivyo sema muone kipigo mtakachopata,kwanza tukijitenga na nyie mtakufa bila maendeleo.

    ReplyDelete
  8. Dini zinaleta chuki, ubaguzi na vita!

    ReplyDelete