Sunday, December 04, 2011

Tanzia - Alfred Ngotezi (Mwandishi wa Habari)

The Late Alfred Ngotezi
Tumepata taarifa kwamba, Mwanahabari mwenzetu, Alfred Ngotezi amefariki ghafla akiwa mjini Arusha usiku huu. Ngotezi ni Mwandishi wa Habari za siku nyingi na alikuwa kifanya kazi hiyo akitokea mjini Mwanza, lakini baadaye akajiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

NSSF wako mjini Arusha kwa ajili ya uenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika (ISSA) ambao utaanza Jumatatu 05.12.2011.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau ndiye aliyetujulisha kuhusu kifo hicho cha Ngotezi na baadaye Meneja Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume pia kutueleza kile kilichotokea.

Ilikuwaje?
Ni kwamba Ngotezi ameanguka ghafla na walipombeba wakitaka kumpeleka hosipitali, tayari alikwishapoteza maisha. Alikuwa anakula, then akaomba bendi impigie muziki, kisha akacheza vizuri tu. Alipomaliza kuburudika aliwapa mikono wanamuziki kama ishara ya shukrani, halafu alirejea kwenye meza na kuketi. Baada ya dakika chache kupita alinyanyuka kwenda chooni, lakini hakufika kwani alianguka kisha kukutwa na mauti.

Kwa wahariri tuliokwenda Tanga, Kagera na Mwanza, mtamkumbuka bwana huyu (Ngotezi) kwa michapo yake na ucheshi wake pia, kwani tulishirikiana naye sana. Ni miongoni mwa walioshiriki sana kazi ya kuratibu suala la mashamba ya mkonge kule Tanga.

Kifo chake ni pigo kwa tasnia ya habari kwani alituwakilisha vyema NSSF, lakini zaidi mchango wake katika sekta ya habari utakumbukwa daima. Pole nyingi kwa familia ya Marehemu Alfred Ngotezi, pole sana Dk Dau na wafanyakazi wa NSSF kwa ujumla na zaidi ya yote poleni sana wana habari wa Tanzania.

Ngotezi umetangulia, wengine tutafuata kila mmoja kwa zamu yake, RIP Alfred Ngotezi.


Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors' Forum (TEF

1 comment: