Saturday, January 14, 2012

Ajali ya Meli Costa Concordia - Titanic 2012

Mwaka 1912 meli ya fahari, Titanic, ilizama katika bahari ya Atlantic.  Titanic iligonga kipande kikubwa cha barafu (iceberg) na sehemu ya chini ikachanywa hivyo maji yaliingia kwa wingi na kusababisha meli kuzama. Watu 1,600 walipoteza maisha yao. Baada ya Titanic kuzama sheria za kusafirsha abiria baharini zilibadilika sana zikizingatia usalama wa wasafiri.


Usiku wa kuamkia leo karibu miaka 100 tangu ajali ya Titanic,  meli ya fahari Costa Concordia imezama kwenye pwani ya Italia. Meli iligonga kitu baharini na sehemu yake ya chini kachanwa. Kwa bahati nzuri ilizama karibu na ardhi. Meli hiyo ilikuwa na wasafiri zaidi ya 4,000. Kati yao watatu wamethibitishwa kufa na 70 wamepotea hawajuliani walipo.

Walioponea ajali  ya Concordia wanasema kuwa zile boat za kuokoa abiria zilikuwa bure maana meli ilizama upande ambao ilikuwa zirushwe majini. Aibiria wengi waliamua kujitosa baharini na kuogelea hadi wafike kwenye ardhi.  


Pia, wanasema kuwa hawakuwahi kufanya zoezi ya jinsi ya kushuka kwenye meli kama ikipata ajali, hivyo watu wengi hawakujua wafanye nini!


Wadau, kila ukipanda kwenye ndege Mhudumu  (au video) anakuonyesha milango ya kutokea ikitokea dharurua na jinisi ya kuvaa zile life vests. Kwenye meli hawafanyi hivyo kweli?


Kwa habari zaidi someni: 


http://www.bbc.co.uk/news/world-europe-16558910

http://www.bbc.co.uk/news/uk-england-dorset-16560737
Meli Costa Concordia baada ya ajali na kabla ya kuzama.



Waokoaji

Meli Costa Concordia ikiwa imelala ubavuni kwenye pwani ya Italia

3 comments:

  1. Spice Islander ingezama karibu na ardhi watu wengi zaidi wangepona. Tatizoo spice ilizama usiku na hapakuwa na mawasiliano.

    ReplyDelete
  2. hiyo meli hapo HAIJAZAMA!imepinduka na kujaa maji ila HAIJAZAMA!kwani sehemu yake nyingine bado ipo juu ya maji.

    ReplyDelete
  3. Kwa lugha ya wanameli mabaharia ni sawa kusema imezama. Hiyo meli haiwezi kutembea tena!

    ReplyDelete