Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika
habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge:
Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.
Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka
kutoa ufafanuzi ufuatao:
Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali
ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.
Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:
Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho
kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika
kulitafakari suala hili.
Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa
cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012
Not surprised. Hii Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu kazi yake ni kukanusha tu. Inafaa kubadilishwa jina na kuitwa Kurugenzi ya Kukanusha ya Ikulu.
ReplyDelete