Nafanya kazi katika Asasi inayotoa elimu ya UKIMWI na Afya ya Uzazi kwa jamii iliyopo Arusha. Mwishoni mwa mwezi huu tulifanya survey ya UKIMWI katika vijiji vya Nanja na Makuyuni vilivyopo wilaya ya Monduli kwa ajili ya mradi tunaotaka kuanza hivi karibuni.
Kilichonisukuma kuandika katika jukwaa hili ni matatizo tuliyoyakuta katika kijiji cha Nanja
HAWANA MAJI
Yaani hakuna kisima wala bomba la maji hivyo hutegemea maji ya mvua ambayo watu wachache ndio wanamatenki ya kuvunia maji hayo. Katika kipindi ambacho si cha mvua hununua maji ndoo ya lita kumi kwa tsh 300 hadi 500.
HAWANA KITUO CHA AFYA
Hakuna kituo cha afya/Zahanati wala clinic ya kutibu wanakijiji. Ikitokea kuna mgonjwa mpaka wampeleke Monduli,Makuyuni au Mto wa mbu ili waweze kupata matibabu. Kwa upande wa kinamama wajawazito wengi wao huzalishwa na wakunga wa jadii hivyo kuna uwezekano mkubwa wa vifo vya mama a mtoto.
Ombi langu kwa wanabidii kama kuna mtu aliyewahi kufanya utafiti au ana uzoefu wa maeneo haya ya Nanja aieleze jamii kuhusu sehemu hii kwakua watanzania wenzetu wanateseka.
Nawakilisha
Malima P. Macha
PM - CHAWAKUA
hawa wananchi wa huko hii shida yao itaisha wakiacha kuendelea kuichagua ccm kama mwakilishi wao.haya mambo kwa maoni yangu yangeweza kushughulikiwa na mbunge wao kama kweli anawawakilisha bungeni.dawa ni moja tu,toa huyo mbunge wa ccm weka chadema nae akishindwa toa weka nccr hadi kuna mmoja atafanya hiyo kazi hata kwa pesa zake binafsi.
ReplyDeleteHili si ndilo jimbo linalowakilishwa bungeni na Edward Lowassa?
ReplyDeleteNi kweli matatizo ya masaini ni mengi,likiwapo la maji.TAWAWAMI,ngo inayofanya kazi Mwanza,imeona hili,na tuko katika hatua za awali kandaa mradi wa maji- visima virefu,10 kwa mwaka 2014,kwa Monduli na Ngorongoro.Wakati ukifika ,tutafika huko monduli,tuone tuanzie wapi
ReplyDeleteDr C S Kivuyo
Agriculture Director
TAWAWAMI-Mwanza