Natoa pole kwa Prof. Mbele ambaye yuko safarini Tanzania ameibiwa LapTop yake. Wasdau mlioko Dar msaidie kuipata!..
******************************************************************************
Nimetua Bongo kutokea ughaibuni tarehe 3 Machi. Wiki moja baadaye,
"laptop" yangu imeibiwa hapa Dar es Salaam, eneo la Sinza. Ilikuwa ni
Apple mpya. Nilikuwa nimeipakia maandishi yangu mengi, miswada na
ripoti za utafiti wa kuanzia 1993.
Ninachohitaji ni haya maandishi. Huu ni mchango wa taaluma ambao natoa
kwa wa-Tanzania na walimwengu. Miswada ya vitabu viwili nilitaka
kuchapisha hapa Tanzania wakati huu, kwa manufaa ya wanafunzi, walimu,
na jamii.
Hii "laptop" ukiifungua inakupa jina la Joseph Mbele, na unahitaji
"password" ili kuweza kuitumia.
Habari ndio hiyo. Hivi sasa najiona kama mkulima mwenye ari ya kulima,
lakini jembe hana. Nakala za miswada ziko ofisini Marekani. Lakini
mimi nilipania kufanya kazi kubwa kwa wiki hizi nitakapokuwa hapa
Tanzania. Nimekwama.
http://hapakwetu.blogspot.com/2012/03/nimetua-bongo-na-laptop-yangu-imetoweka.html
pole profesa kwa matatizo hayo...ushauri kidogo;mi nafikiri useme hiyo password hapa ili huyo mwizi aweze kukopi data zako ktk disc na useme akutumie wapi.Haina maana ya kuficha hiyo password kama bado unataka data zako kwani kama huyo mwizi akimtafuta mtaalam wa computer ku-reset hiyo password sio kazi kubwa...
ReplyDeletePole prof, lakini ina maana hukuwa na backup? Ni hatari sana mtu kuweka nyaraka muhimu katika kompyuta bila kuwa na backup kwa sababu anything can happen. This is especially true with laptops ambazo watu huenda nazo huku na kule.
ReplyDeleteWadau, shukrani kwa mawaidha yenu. Mugo, wazo la kuianika password ili kibaka aione imenipa mtihani mkubwa :-)
ReplyDeleteIla kama unavyosema, wadau hapa Dar wameniambia kuwa mafundi wanaweza kabisa kufanya maarifa ya kuingia katika hizo kompyuta. Kwa vile hii si taaluma yangu, nimepata elimu hapo.