Baraza la Habari Tanzania: Acheni Mahakama Ifanye Kazi Yake Juu Ya Kifo Cha Steven Kanumba
KAMATI ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) leo mchana imetangaza imesikitishwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili uliojitokeza hivi karibuni kwa baadhi ya vyombo vya Habari ambavyo wakati vikiripoti kuhusu kifo cha Msanii Steven Charles Kanumba, vimemhukumu msichana Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu, kuwa amemuua msanii huyo.
Ukiukwaji huo umejitokeza hasa baada ya msichana huyo kufikishwa Mahakamani, ambapo baadhi ya magazeti yanayoheshimika katika jamii jana Alhamisi, Aprili 12, 2012 yaliandika vichwa vikubwa vilivyosomeka: Lulu Kortini kwa kumuua Kanumba na Lulu Kizimbani kwa mauaji ya Kanumba.
Kwa mujibu wa sheria na maadili ya Uandishi wa Habari mtu yeyote anayekamatwa kwa tuhuma yoyote ile ni mtuhumiwa mpaka atiwe hatiani na mahakama.
Kanuni hii ya siku nyingi katika fani ya uandishi wa habari inafahamika na waandishi na wahariri wote wanaoheshimu kazi yao.
Baraza pia limeshatoa matamko mara kadhaa kuwakumbusha wanahabari kujiepusha na uandishi wa habari au vichwa vya habari vinavyohukumu.
Baraza linafahamu fika kuwa kesi zilizoko Mahakamani ni kivutio kwa umaa kutaka kujua kinachoendelea ili kuona haki ikitendeka na pia wanahabari wana haki ya kujua na kuripoti yanayojiri huko na katika vyombo vingine vya sheria.
Lakini lazima ifahamike kuwa wakati wakitumia fursa na haki hiyo Wanahabari wanapaswa kuzingatia kanuni, miongozo na sheria zinazolinda haki za msingi zxa watuhumiwa na uhuru wa Mahakama.
Ni wazi kuwa vichwa vya habari vilivyoitajwa hapo juu vimeliingilia uhuru wa Mahakama kwa kuchapisha habari ambazo zinaonekana kushawishi au kushinikiza uamuzi wa Mahakama.
Wanahabari ni lazima watambue kuwa kuna taratibu na makubaliano ya kijamii juu ya namna gani taarifa zinavyopaswa kuripotiwa ili kutowadhuru watu wengine.
Hivyo basi , Baraza la Habari Tanzania linapenda kuwakumbusha tena wahariri kuhakikisha kuwa wanafanya kazi yao kwa kuzingatia maadili na weledi katika kuripoti mkasa huu unaogusa hisia za watu.
Imesainiwa na
Jaji Thomas B. Mihayo
Mwenyekiti
Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania.
Mimi sijawahi kuona mtuhumiwa akitetewa kwa nguvu namna hii na pia kulindwa na serikali yenyewe.
ReplyDeletehata waandishi wa habari wamenyimwa fursa ya kumwona.
Halafu kuhusu huyu Lulu amekuwa akidanganya umri wake mara kadhaa. Kwa hiyo hana sifa za kuaminika.
Sasa inawezekana kuna mkono wa mtu mwingine pia katika kifo hiki.
Sasa kuna haja gani ya kutafuta mkono mwingine kama wote tumeaminishwa Lulu ndiye mhusika? Baraza liko right.
DeleteHatua hii haitoshi. Vyombo vya habari husika viwajibishwe kwa kuingilia mwenendo wa kesi
ReplyDeleteYes, Baraza liko sahihi kabisa. Tatizo ni kwamba vyombo vya habari Bongo sasa vinategemea sensationalism na outright lies ili kujiuza na kujaribu ku-survive katika soko lenye ushindani mkali. Kwa mfano ni leo tu kuna gazeti limedai Kanumba ameonekana mitaani akinunua vocha ya simu. Baraza hapa limezungumzia very basic journalism ambayo mtu huhitaji kuwa na PhD kuifahamu. Hata mimi sikutegemea magazeti kama Mwananchi na Nipashe kuandika headline ambazo zinaonekana kama zimeandikwa na watu ambao hawajawahi kutia mguu katika shule ya uandishi wa habari.
ReplyDeleteTunapoongelea mkono mwingine tunamaanisha "She "Lulu" had accomplices".
ReplyDeleteAma inawezekana she was being used by a third party. By the way the "caller" may be the accomplice who may have been signalling for the operation to commence.
Mnajuaje kasukumwa,yet you were not there during the incidence? Things happen,ni ajali,dont blame on lulu...she may be innocent,the fact that she were last seen with the great steve(rest in peace our hero),doesnt make her responsible for his death.
ReplyDeleteBy a journalist from Kenya
Magazeti yanamwekea Mtoto Lulu katika mazingira magumu hasa kama akishinda kesi nayo yamesha mtaja kuwa ni muuaji. Naomba baraza liyaadhibu magazeti hayo.
ReplyDelete