THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
MAWAZIRI
1. OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,
2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,
3. OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
4. WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa Ujenzi
Dr. John P. Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,
Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,
5. NAIBU MAWAZIRI
OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI
6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,
7. OFISI YA WAZIRI MKUU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
8. WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,
Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Mei, 2012
Rais Kikwete akitangaza baraza alilolisuka upya amesema au kudokeza kuwa Tanzania sasa inayo mafuta.
ReplyDeleteIngawa watu wengi tumevutiwa na uteuzi wa mawaziri na kusahau taarifa hizi rasmi, kuna umuhimu taarifa zaidi tuzipate kuhusu mafanikio haya ambayo yanaweza kuleta matumaini ya uchumi mzuri kwa taifa kama sio balaa (oil curse).
Uvumbuzi huu utapelekea wizara ya Madini na nishati kugawanywa na kuwa wizara mbili kwenye bajeti ijayo.
Kuna sura mpya ambazo hazikuwahi kuonekana hapo kabla.
ReplyDeleteKuna watu ambao mchango wao kwa taifa na kwa ulimwengu huu unaheshimika jambo linalonifanya binafsi niamini kuwa hata kwa nafasi walizopewa watafanya mambo mapya mazuri kwa watz.
Mawaziri Wapya ni Mwakyembe - Uchukuzi, Abdalah Kigoda - Viwanda na Biashara, Mgimwa - Fedha, Kagasheki - Maliasili; Dkt. Fenela - Habari; Chiza - Kilimo,
ReplyDeleteManaibu niliowapata wapya ni Saada Mkuya - Fedha; Simbachawene - Nishati; Makamba - Sayansi&Teknolojia; Benelith Mahenge - Maji&Uvivu; Masele - Madini; Angela Kairuki - Katiba; Janeth Mbene - Fedha; Makala - Habari; na Dkt Seif Rashid - Afya
Kama JK amewaondoa ina maana tuhuma zao zilikuwa ni za ukweli. Sasa kama wameiba wanatakiwa warusishe na wakiri kwa watanzania wote kwamba walituibiwa. Kuachwa tu ina maana hata hao waliongia wanaweza kula alafu wakaachwa lakini wameshajinufaisha bwana. So tukiwaka utamaduni wa kuwajibishana inakuwa powa zaidi ili mtu ajue kuwa hata akifukuzwa bado atawajibishwa pia.
ReplyDeleteHii ni nzuri jamaa waligoma kujiuzuru wakitegemea huruma ya Kaka Mkuu lakini kawatosa, Kinachofuata ni kwamba hawa jamaa wafikishwe Mahakamani na mikataba walioingia pale penye maslahi yao pabomolewe.
Wamezdi!!!
ReplyDelete1. BARAZA NI KUBWA MNO- ( toka 50 hadi 55) hapa tunaongea kuongezeka kwa magari mapya matano, mishahara ya mawaziri wapya watano, posho kwa watu wapya watano, bila shaka watapewa na wasaidizi nyumba na umeme wa bure na wataongeza kiasi cha pesa ya serikali inayopotea
2. SURA ZILEZILE - baadhi ya matu waliorudishwa ni wale waliokuwepo wakavurundaau wengine wamerudi kwenye utamaduni wa zamani haribu hapa utapewa sehemu nyingine. Sitegemei Maghembe, Kombani, Malima walete mabadiliko wanajaza nafasi tu
3. KUTOKUZINGATIA SHERIA - Tunategemea kama kawaida kutakuwa na semina elekezi nyingi, Mimi nashangaa ni Magufuli peke yake anayesoma sheria na
kuzisimamia wengine wanakuwa na visingizio kibao. Kwa ufanisi anaokuwa nao Magufuri kila nakoenda inaonesha wizara zote zina utaratibu mzuri wa kuleta tija ila wanaoteuliwa kuzisimamia wanaenda kuuza sura tu.
Nategemea haya mambo matatu yameleta dosari kubwa katika baraza zima la mawaziri ukizingatia kuwa Kaka Mkuu alisema kuongeza mshahara kwa wafanyakazi kunategemea sana makusanyo wakati kuna watu wanachukua makusanyo yote kupeleka nyumbani kwao bila hata kuchangia kujenga barabara ya mtaa itaka kuwakomoa majirani.
Naamini hili baraza litavunjwa tena kabla ya mwisho wa mwak huu.
Huu ni upuuzi nakubaliana na Mdau aliyesema Baraza ni kubwa na mimi nasema ni Mzigo kwa Walipa Kodi.Huu mfumo umepitwa na wakati Wizara nyingine hazina maana,mfano Utawala Bora,toka wizara hii ianzishwe nchi imeingia mikataba mibovu kibao,ufisadi na wizi.Hii kutokana na KATIBA MBOVU iliyopitwa na WAKATI ambayo haina MANUFAA kwa WANANCHI.Karne hii ya 21 hatuhitaji BARAZA la mawaziri,manaibu,makatibu wakuu wote hawa,pesa zote za kodi zinaishia kwenye matumizi.
ReplyDeleteNakubaliana na Sefu Saidi Watawala wetu nivichekesho baraza toka 50 hadi 55 nisawa na mtu anayebeba mzigo wa kuni mzito anaposhindwa anautua chini badala ya kuupunguza anaongeza kuni zaidi nakujaribu kuubeba tena.Watawala acheni kuiga ya utawala wa nchi kubwa nchi kubwa ni sawa na bara lote la Africa wakati nchi yenu nisawa na Majimbo tuu.Waswahili wanasema JIKUNE unapofikia.
ReplyDelete