Dear All,
Information from the Tanganyika Law Society regrets to announce the untimely death of Prof. Michael Wambali of the School of Law(Formerly Faculty of Law)
Prof. Wambali has passed on a few minutes ago at Muhimbili National Hospital.
Those who knew him have lost a teacher and a friend. The nation has, without doubt lost a legal luminary.
May his soul rest in eternal peace.
MJL
RIP indeed. And strength to all his family.
ReplyDeleteTo be personal for a moment ... three of my greatest students and friends, Prof Mwaikusa, Prof Wambali and Ibrahim Ngozi, all Milambo 1974, all dead. Too soon jamani much much too soon
Rafiki yangu na mwanadarasa wangu Prof. Michael Kajela Beatus Wambali amefariki dunia leo tarehe 4.4.2013. Kwanza alilazwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kabla ya juzi kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikofariki dunia. Kwanza ilisemwa kuwa Prof. Wambali alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu. Baadaye,ikasemwa kuwa Prof. Wambali amegundulika kuwa na uvimbe sehemu ya koromeo uliokuwa ukiathiri ulaji wake. UDSM kama mwajiri wake ilishindwa hata kumpatia huduma ya haraka Prof. Wambali. Jibu lililotoka UDSM na kuidhinishwa na Kitivo cha Sheria pale lilisema kuwa 'Chuo Kikuu hakina hela'. Prof. alipaswa kufanyiwa matibabu ya haraka hapa nchini,nchini Afrika Kusini au India. Akaachwa.Akasuswa. Hata Prof. Wambali amefanyiwa hivyo kweli? Chuo kimekosa fedha za matibabu kwa Mhadhiri tegemezi wa Sheria kama huyu? Chuo kina fedha nyingi kulipa safari za Prof. Mukandara na watu wake na si matibabu ya wahadhiri wake? Inauma sana na kutia aibu. Nenda Prof. Wambali. Lakini,UDSM watalaumiwa kwa kukutelekeza pamoja na huduma iliyotukuka uliyowapatia tangu miaka ya 80 hadi leo. Msalimu Comrade mwenzetu,Hayati Prof. Jwan Mwaikusa. Pumzika kwa amani classmate! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
ReplyDeleteWanasiasa wakishinikiza kupelekwa India au South Africa kutibiwa mafua, lakini nalaumu hawa wataalamu wetu waliojikataa kukosa kuhakikisha wanahamasisha kutoa uelewa mpana kwa wananchi kwamba haki ya matibabu kuishi ni ya wana CCM na viongozi wa serikali ya CCM, rejea yule mama mwenye uvimbe mkubwa wa mguu, Tende aliyepiganiwa sana na ITV hivi yule amam bila chombo cha habari jee angekuja kuona uhalari wa maisha kweli
ReplyDeleteR,I.P. Prof , uliowajaza wananfunzi wako yataendelea kubaki vizazi na vizazi !
Prof. Michael Kajela Beatus Wambali amefariki jana. Ni pigo kwa UDSM;kwa familia yake,ndugu,jamaa na rafikize. Na hata kwetu wanafunzi wake pale Kitivo cha Sheria-UDSM.
ReplyDeleteKama Mhadhiri mbobezi
Namkumbuka Prof. Wambali kama Mhadhiri mbobezi katika nyanja ya Sheria. Prof. Wambali aliyeanza kuhadhiri UDSM tangu mwaka 1982(mwaka niliozaliwa) kama Mhadhiri Msaidizi,alikuwa mbobezi wa sheria za kimataifa,za katiba,za utawala na za madai kwa ujumla. Prof. Wambali alipata cheo na hadhi ya kuwa Profesa Mshiriki mwishoni mwa mwaka 2011. Alipata Shahada yake ya kwanza ya Sheria mnamo mwaka 1981 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Baadaye akapata Shahada za Uzamili na Uzamivu katika miaka ya 1984 na 1987 katika vyuo vya UDSM na Warwick.
Kama Mhadhiri wangu
Nilipojiunga UDSM kwa masomo ya Shahada ya Kwanza ya Sheria mwaka 2005,nilimkuta Prof. Wambali.Nilibahatika kufundishwa somo la Sheria za Ushahidi naye nikiwa mwaka wa pili wa masomo chuoni hapo. Mwaka 2007 tena Prof. Wambali alituhadhiri katika Sheria za Utafiti.
Kiukweli,ni mhadhiri kweli. Sauti yake ya utulivu lakini ya kiuhadhiri ilipenya vyema masikioni mwetu kama wanafunzi wake. Tulipata tulichokipata. Kwa kila aliyefundishwa naye,naamini anapata taabu kutafuta makosa ya kiweledi na kiuerevu ya Prof. Wambali.
Kama Mhadhiri Mzazi
Mara zote Prof.Wambali alitufundisha kuwa na misimamo,uelewa wa mambo na kujiamini. ' Msiongee kama mko vyumbani na wapenzi wenu.Ongeeni kwa sauti ili msikike kama Wanasheria' alipenda kutania kimazungumzo Prof. Wambali. Alituongoza kama baba,mlezi na mjuzi wa sheria Kitivoni.
Kama Mbobezi wa Sheria
Kwa hilo sina mengi sana ya kuzungumza. Tangu mwaka 1982 amekuwa Mhadhiri wa UDSM. Mwaka 1986,Prof. Wambali alikuwa Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na zile za chini kwayo. Alikuwa mtetezi wa wateja wake asiyetetereka na mwenye kufanya tafiti za kisheria kabla ya kuchagua upande wa kisheria wa kuusimamia.Alibobea hadi akapitiliza.
Natoa pole
Natoa pole kwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria-UDSM,Prof. Bonaventure Ishengoma Rutinwa na Kitivo kizima,Makamu Mkuu wa UDSM,Prof. Rwekaza Sympho Mukandala,wafanyakazi wote wa UDSM,familia ya Prof. Wambali,ndugu, jamaa, rafiki wote na wanafunzi wake wote popote walipo. Na hata Tanzania nzima kwa kumpoteza Prof. Wambali.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi. Amina.