Father Urbanus Ngowi Phooto from Catholicweb.com |
Father Urbanus Ngowi afumaniwa na Mke wa Mtu akivunja amri 10 Mjini Moshi
KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lina sakata zima.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!
Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.
“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe (jina tunalo) alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.
Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.
“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”
AWEKWA KITIMOTO
Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.
Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.
Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake!
SIKU ZA NYUMA
Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.
Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo alizosema zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.
Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.
IJUMAA WIKIENDA NA FATHER NGOWI SASA
Baada ya kujazwa madai hayo, kama ilivyo desturi ya Magazeti ya Global Publishers likiwemo hili (Ijumaa Wikienda), lilimsaka Father Ngowi kwa udi na uvumba ambapo Ijumaa iliyopita nyakati za mchana lilifanikiwa kuzungumza naye lakini kabla ya kufanya hivyo, kifaa cha kunasia sauti kiliwekwa sawa na mambo yalikuwa hivi:
Wikienda: Haloo, naongea na Father Ngowi wa Parokia ya Korongoni, Marangu, Moshi?
Father Ngowi: Naam ni mimi, nani mwenzangu?
Wikienda: Naitwa…(mhariri anataja jina), napiga simu kutoka Magazeti ya Global Publishers.
Father Ngowi: Uko wapi?
Wikienda: Makao Makuu ya Global Publishers, Dar es Salaam.
Father Ngowi: Eeh…unasemaje?
Wikienda: Kuna madai ya wewe kukutwa na mke wa mtu chumbani. Je, unaweza kunielezea kama ni kweli na tukio lilikuwaje?
Father Ngowi: Siyo mimi.
Wikienda: Wewe siyo Father Urbanus Ngowi?
Father Ngowi: Nimekwambia siyo mimi, hao ni matapeli wanataka pesa ndiyo wametengeneza hizo picha.
Wikienda: Kwa hiyo unataka kuniambia hizi picha ni za kutengeneza?
Father Ngowi: Nimekwambia hao ni matapeli wanataka pesa.
Wikienda: Ulishaziona picha zenyewe?
Father Ngowi: Sijui.
NGOMA YATUPWA KWA MKUU WA JIMBO
Wikienda: Mbona tayari tukio hilo linadaiwa limeshafika kwenye ngazi ya jimbo, Moshi kwa Father Paul Uria?
Father Ngowi: Muulize yeye ndiye mkubwa wangu.
Wikienda: Basi nisaidie namba yake ya simu ya mkononi.
Baada ya takribani dakika 10, Father Ngowi alituma namba ya simu ya Father Uria na mambo yakawa hivi:
Wikienda (huku kinasa sauti kikiendelea kufanya kazi): Haloo…naitwa …(mhariri anajitambulisha) kutoka Magazeti ya Global Publishers, Dar es Salaam, naongea na Mkuu wa Jimbo Kanisa Katoliki, Moshi, Father Uria?
Father Uria (kwa sauti yenye unyenyekevu): Ndiyo.
Wikienda: Una taarifa za mtumishi wako, Father Ngowi kunaswa na mke wa mtu chumbani?
Father Uria: Kwanza mimi si mkuu wa jimbo, ni mwakilishi wa mkuu wa jimbo. Sipo mjini kwa sasa nipo Kilema huku vijijini kwenye huduma lakini nilikuta ‘missed calls’ zake jana (Alhamisi) kwani ilikuwa tukutane kwa sababu alishanijulisha kuwa kuna tukio kama hilo unaloniambia wewe.
NGOMA YAWA NZITO, YATUPWA LEO JUMATATU
“Kweli tulikuwa tukae jana lakini ikashindikana, leo (Ijumaa) ni sikukuu (Muungano), kesho (Jumamosi) na keshokutwa (Jumapili) ni wikiendi. Kwa hiyo tutakaa Jumatatu (leo) hivyo nipigie saa 10:00 jioni siku hiyo ili nikupe maagizo tutakayofikia na mengine.
Wikienda: Lakini Father Ngowi alikueleza tukio lilikuwaje?
Father Uria: Nimekwambia tukikaa ndiyo tutajua kilichotokea. Wewe nipigie hiyo saa 10 nikupe kitakachojiri.
Wikienda: Shukrani Father Uria kwa ushirikiano.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
Father Ngowi na Mama P wakiwa na nyuso za aibu baada ya Kufumaniwa! |
Huyo mwenye mkee amshtaki father Ngowi kwa kosa la kumtafunia mke wake bila idhini yake anaweza pata fungu zuri toka Kanisa Katoliki au aombe appointment ya kumwona papa amweleze yaliyojiri!
ReplyDeleteNamkumbuka father Ngowi sina kumbukumbu halisi ya mwaka ila ni kati ya 2001-2003 akiwa parokia ya olele iliyoshawahi kuwa kigango cha Mashati mkuu rombo,father Ngowi alichomwa na kisu tumboni na watu wasiofahamika huku tetesi zikiwa ni kwa sababu alikuwa anatembea na mke wa mtu.
ReplyDeleteNakumbuka tulifanya maandamano ya amani kulaani kitendo alichofanyiwa padri wetu huyu na watu tulilia mno tukiwa na imani labda wauza gongo ndo wamefanya hivyo sababu alikuwa akiwalaani na kudeal nao mno.
Habari hii imenishtua mno,naamini na waumini wa parokia ya Olele kule Mashati rombo wakisikia habari hii watahuzunika zaidi.
Enyi mapadri wetu wapendwa,upadri ni wito kama hauuwezi wito huo achana nao..tumechoshwa na vitendo vya aibu mvifanyavyo.
Mpendwa kadrinali Pengo...uko wapi baba mbona haya matukio ya mapadri wetu yanapamba moto sana kipindo hiki jamani?? Do something ulinusuru kanisa..
Jamani si waruhusiwe waoe tu alitaka afanye kama daudi na Uria ale uroda halafu uria mhiti angie kwa mkewe akishika mimba ionekana ni ya uri amhiti kumbe padre!!! waoe ili wacha ukware wako wengi kweli
ReplyDeletewote ni watu wazima shida nini? nyie binadamu muache kuhukumu wenzenu angekua mtoto na mimi ningesapoti lakini haya maswala ya kuwafata watu wazima wawili wanaofanya mapenzi kwa hiari yao sio mazuri muache mungu awahukumu na nyie binadamu mfate yenu huo ni umbea tu hakuna lingine wewe mume mkeo anakusaliti ni dalili hakupendi wewe usipoteze muda wako kumuaibisha na kuaibisha familia yako tafuta anayekupenda na wewe uishi kwa amani huyo padri muacheni sheria zichukue mkondo na nyie mashemeji mkawapende wake zenu acheni kufatilia maisha ya ndugu yenu
ReplyDelete