Wadau, mnaweza kuniona nyuma ya mcheza sinema maarufu, Amy Adams katika trela ya sinema mpya American Hustle. Inatoka mwezi Desemba. Niliigiza mwezi wa pili mwaka huu. Waliomba wacheza sinema wasio na miili ya stars kujitokeza kwa ajili ya hii scene ya party. Nilituma picha nimevaa nguo ya kuogelea na wakanichagua. Awali ilikuwa nivae bikini lakini kutokana na urithi wa bibi (matiti makubwa) walishindwa kunipatia nguo iliyofaa. Sehemu ya chini ilikaa viuri lakini juu ziilikuwa ndogo hadi matiti yanamwagika! Basi, wakanipatia hiyo one piece nyeusi na ndo nilivaa. Ajabu siku tulivopiga sinema nilidhani kuwa sitaonekana hata kidogo. Pia ilikuwa winter na kulikuwa na theluji na barufu nje! Leo asubuhi, nilishangaa watu walipoanza kunipigia simu na kunitumia text kuwa wameniona. Kumbe hiyo sehemu imeongelewa na kuonyeshwa sana kwa vile Amy Adams kavaa nguo ya kuogelea ilitengenezwa kwa mkono kwa mtindo wa macrame. Katika sinema hiyo naonekana katika scene hii moja tu kwenye bwawa ya kuogelea kwenye nyumba ya tajiri fulani hapa Boston. Waigizaji wote tulizuiliwa kusema kitu, yaani tumefanya nini na tumeona nini. Tulisaini agreement za usiri. Sasa tunaweza kusema.
HONGERENI SANA, NATAMANI VISA VYANGU VIJE VIIGIZWE SINEMA, NI NDOTO YANGU ...
ReplyDeleteSafi sana Da Chemi. It's good to see that you are going places. Hongera.
ReplyDeleteNimeipenda shepu ya huyo jamaa aliyenyanyua mikono.
ReplyDeleteHongera Dada Chemi!
ReplyDeleteCONGRATULATIONS sis!
ReplyDeleteDuh! Safi sana. Utafika Dada Chemi!
ReplyDeleteMi manyonyo makubwa ndo ugonjwa wangu.
ReplyDelete