Marehemu Erasto Msuya, alikuwa bilionea. Mnashangaa nini jeneza lake likifunguliwa kwa remote control? Rest in peace.
*************************************
Kutoka Gazeti la MWANANCHI:
Arusha - Mazishi ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu Erasto Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalotumika kubeba mwili wake linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’.
*************************************
The late Tanzanian Billionaire Erasto Msuya. He was murdered. |
Kutoka Gazeti la MWANANCHI:
Arusha - Mazishi ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu Erasto Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalotumika kubeba mwili wake linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’.
Msuya aliyeuawa wiki iliyopita, anazikwa leo huku
familia ikitangaza kutokulipiza kisasi kwa waliohusika, badala yake
wamemwachia Mungu.
Kinachovutia katika msiba huo ni jeneza lililobeba
mwili wa mfanyabiashara huyo lililoagizwa Nairobi, la aina yake huku
likifunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.
Jeneza hilo lililoagizwa kutoka Kampuni ya
Montezuma & Monalisa Funeral Home, linafunguliwa kwa kubonyeza kifaa
maalumu hata mhusika anapokuwa mbali.
Hali hiyo ilionekana kuwaacha na mshangao maelfu
ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada iliyofanyika
nyumbani kwake, Kwa Iddi, wilayani Arumeru.
Mfanyabiashara huyo aliyeuawa kwa kumiminiwa
risasi zaidi ya 20 na watu wasiojulikana, anazikwa leo nyumbani kwao
eneo la Kairo Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.
Kaka wa marehemu, Israel Msuya, alisema jana kuwa
mazishi hayo yatafanyika makaburi ya familia ya mzee Elisaria Msuya
‘Kikaango’, baba wa marehemu Erasto.
Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya mazishi hayo
inayoongozwa na kaka mkubwa wa familia ya Msuya, Gady, zaidi ya Sh100
milioni zimepangwa kugharimia shughuli za maombolezo na mazishi.
Jeneza na gari maalumu la kubebea mwili wa
marehemu yameagizwa kutoka Kampuni ya Montezuma & Monalisa Funeral
Home ya Nairobi, Kenya kwa gharama ya Sh8 milioni.
Chakula, vinywaji, mapambo na magari ya kukodishwa
kutoka Arusha kwenda Mirerani na kurudi yanatarajiwa kugharimu zaidi ya
Sh80 milioni.
Katika hatua nyingine, polisi mkoani Arusha
imeendelea kuwahoji wafanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite wa
Mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro, wakidaiwa kuhusika na kifo
hicho.
Habari zilizopatikana jana zinadai mfanyabiashara
mmoja kijana ambaye aliibuka ghafla kuwa tajiri mkubwa kutokana na
biashara ya madini ya Tanzanite, anashikiliwa Arusha kwa mahojiano.
Jana, kwenye viunga vya Mji wa Mirerani watu walitangaziwa kuwa
mfanyabiashara huyo, alikuwa anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na
kifo hicho.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha,
Liberatus Sabas, hakupatikana mara moja kuelezea suala hilo kwani simu
yake ilipopigwa ilikuwa haipatikani.
Marehemu ameacha mke na watoto wanne, huku akiacha
rasilimali nyingi ikiwamo jumba la kifahari lililopo Sakina kwa Idd,
hoteli maarufu za SG Resort na Mezza Luna zilizopo Arusha.
Na hata kabuli lake pia lichimbwe kwa kutumia rimoti kontrol.
ReplyDeleteOMG! Wonders never cease! To think that all this (obscene wealth, extravagance, and opulence) is in a country where some people don't even have clean drinking water!
ReplyDeleteAll the same, nobody deserves to be murdered, ie no human being has the right to kill another. REST in PEACE Mzee Msuya.