TAMKO
LA JESHI LA POLISI TANZANIA KUHUSU
SAKATA LA SHEKHE PONDA
1. MNAMO TAREHE 10,
AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA
NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA EID
LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA
KONGAMANO HILO KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA
KWA MUDA MFUPI.
2. KONGAMANO HILO
LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI
YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA
KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE
KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA
LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA
KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.
3. BAAADA YA ASKARI
KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA MAWE
ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA
KUWATAWANYA.
4. KATIKA VURUGU
HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI SASA IMETHIBITIKA
KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA
KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.
5. KUFUATIA TUKIO
HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA
KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA
TUKIO HILO.
6. AIDHA, JESHI LA
POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI
LINASHUGHULIKIWA KISHE
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la
Polisi.
ReplyDeleteHivi , Polisi mnafikiri nini kabla ya kutoa haya na matamko yenu? Hivi hii inatosha kuwatuliza wananchi kwa njia mliyoandika? Ham semi kama akipiga risasi na polisi au ni her aha l kiwe au panga,
Ripoti ya bomu la Arusha iko wapi , na huyu Mungulu alikuwa huko? Nachoka kabisa