Kwa mara ya kwanza Nchi mbili za Afrika zinawakilishwa katika Tuzo za Juu za Oscars.
Lupita Nyong'o yuko katika Best Supporting Actress (yaani mwigizaji bora wa kike katika sinema si mwigizaji mkuu). Na Barkhad Abdi anagombea Best Supporting Actor (yaani mwigizaji bora wa kiume - si mwigizaji mkuu).
Jamani, jamani sijui waafrika tukoje, huyo Barkad kasemwa na waSomali wenzake, eti ana sura mbaya na mengine! Khaa!
Na nisimsahahau Chiwetel Ejiofor ambaye ni Mwingereza mwenye asili ya Nigeria. Yeye anagombea Mwigizaji bora wa kiume. (Best Actor).
Kushoto ni Lupita Nyong'o na Kulia ni Barkhad Abdi |
Mara nyingi nchi ya Afrika inayopata sifa katika Osars ni Afrika Kusini. Waigizaji wao wazungu kama Charlize Theron wanatambulika sana. Charlize alikuwa Msouth Afrika wa kwanza kupata Oscar.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:
Congratulations LUPITA!
ReplyDelete