Mdau TJK ameleta hoja hii. Mnasemaje wadau? Je, ni kweli hao barabershop girls wanavunja ndoa za watu? Navyoona midume ndo inashindwa kujizuia!
******************************
Mwanzo ilikuwa ni vita na wahudumu wa bar. Wanawake walio kwenye ndoa
waliishi kwa hofu ya ndoa zao kuingiliwa na wadada warembo wanaovaa nusu
uchi kweye bars zilizopo karibu kila sehemu ya Dar es Salaam. Lakini sasa,
mambo yamehamia kwenye babaershops/salon za kiume.
Nadhani kila mtu anajua babershop ni nini, na pia anajua barbershop za siku
hizi sio kukata nywele peke yake,bali
inajumuisha angalau lisaa limoja la
kufanyiwa scrub, massage, manicure, pedicure etc.
Tunajua wasichana hao wakati wa kutoa huduma hawawezi kuepuka kugusa wateja
wao so gently usoni wakati wa kufanya scrub na massage. huduma wakati
mwingine huenda zaidi ya huduma za kinyozi , wakati mwingine wateja
wanauliza kukutana na wasichana hawa baada ya saa za kazi. " Wakati
mwingine wasichana hulipwa fedha za ziada kwa kisingizio cha kuthamini
huduma waliyotoa.
Barbershops nyingi zimegeuka kuwa mahala pa biashara ya ngono. Wanaume
hawana muda tena na wahudumu wa baa, na hii ni tishio kwa ndoa nyingi hapa
mjini.
Je unalo la kusema kuhusu hili? Karibu tujadiliane!
Mwanaume wa aina hiyo hajithamini.
ReplyDeletena hapo "pakujithamini" panahitaji pia mjadala mrefu.
ReplyDeleteKwa ujumla maisha ya vijana tanzania ni magumu, kila siku wanatafuta namna ya kupata ujira, wanawake wanaosha vipara tena bila kuwa na vifaa vya kinga kama gloves.
Wavulana nao wanafanya kazi za kuosha miguu ya akinamama na kusuka mawigi.
Lipo kundi la wapiga debe, waendesha bodaboda, waokota makopo na vyuma chakavu yaani tabu kwa kwenda mbele.
Tumejenga shule za kata kuandaa wauza mpesa, ndiyo ajira iliyosalia kwa waliopata ziro na four.
Vyuoni vijana wanachacharika kuwafanyia asingment wazee waosha vyeti kwa ujira wa sahani za wali.
Vijana wa maofisini akiingia tu anataka awe na kivitz achane na adha ya kushikwa makalio kwenye daladala, kimbembe kwenye foleni za dar bila wese la buku teni hajaenda kazini achilia kamkopo ka bank, basi kutwa nzima kurusha sms akipiga mizinga.
Wajumbe wetu vijana nao siku nzima wanaomba miongozo angalau waonekane kwa tv manake hakuna walichofanya majimboni.
There are people in various professions or jobs where they handle the human body; eg doctors, nurses, physiotherapists, hairdressers, barbers, beauty therapists, masseurs, etc.
ReplyDeleteThe thing for people to remember, is that these people are merely doing their jobs (be it that they touch/ or manipulate other people's bodies, for various treatments, therapy, etc). They are NOT doing their jobs as a means to SEXUAL FAVOURS or sex trade.
This dirty new trend in the nasty behaviour of male customers in Dar's barbershops shows how SHALLOW and RIDICULOUS their ATTITUDES are; besides their actual BEHAVIOUR. Damn backward and SEXIST! Stupid to the max! What happened to look, but DO NOT TOUCH? Admire, but then leave it alone! Yeah?!
In the old days, besides fondling barmaids, some men went as far as fondling NURSES, who were there to treat them/ nurse them back to health. Damn!
Some people THINK with the CONTENTS in their UNDERWEAR, instead of thinking with what's in their heads- BRAIN! Where's their SELF-RESPECT and RESPECT for others? Goodness gracious me!
Hakuna heshima wala adabu! Wanaume wanaofanya upumbavu huo, ni wajinga, wachafu, na washamba!
ReplyDelete"JE, KWELI HAO BARBERSHOP-GIRLS WANAVUNJA NDOA ZA WATU?"
ReplyDeleteHapana Hapana Hapana! Wanauovunja ndoa ni wanaume wenjeye, ambao wanatamaa za kuingia ndani ya chupi za wanawake wasiokuwa wake zao. Hawashibi wala kutosheka. Tamaa zina matokeo mabaya! Uroho Uroho Uroho was dhambi!
Ole wao wenye uroho na tamaa! Ukmwi/ HIV na AIDS inawangoja katika kila kona. HIV-AIDS haibagui!
Kuowaona wahudumu ya kike wa barbershops kama sex objects ni kuwadhalilisha. Ukienda barbershop basi fuata huduma inayotolewa hapo, si kuwaza ngono. Kama ni ngono, wapo wanawake tele wanaojiuza mitaani na kwenye mabaa.
ReplyDeleteNyie manasema nini, niliona siku moja nikabaki na maswali mengi bila majibu. Mnajua sehemu ya shingo ya mwanaume ni moja ya maeneo so sensitive, sasa weye binti umekazana unamfanyia mwanaume asiyewako massage maeneo kama hayo unataka nini? Labda kutoelewa kwa hawa mabinti lakini kwa kweli ni hatari, kitu wanachofanya kwa aliyekamilika ni kuchokoza hisia za uzinifu. Na nyie kina baba msikubali kufanyiwa massage hata oshwa nywele kwa kinyozi maana hisia zenu za mwili zipo kwa ncha ya kidole
ReplyDelete