Mbeya
Vijijini
BAADHI ya
akinamama na wanakijiji wa baadhi ya vijiji vya Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya
Vijijini wamewalalamikia wauguzi na wahudumu wa afya katika Kituo cha Afya Simambwe
kwa kile baadhi yao kuwaomba kitu kidogo (rushwa) hasa kwa wajawazito
wanapofika katika kituo hicho kupata huduma.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake kutoka vijiji vinavyohudumiwa na kituo
hicho vya Usoha Njiapanda, Shibolya, Simambwe, Garijembe, Ilembo Usafwa, Ngoha
na Zunya walisema mjamzito amekuwa akiombwa kutoa shilingi 2000 kila
anapojifungulia nyumbani kwa dharura baada ya kushindwa kufika katika kituo
hicho.
Mmoja wa
akinamama aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi ambaye aliomba kutotajwa
kwa kuwa huenda akapata taabu kihuduma za afya kituoni hapo, alisema kwa sasa
ni jambo la kawaida wahudumu kuwaomba chochote wajawazito kituoni hapo.
“…Unajua
vijiji vingi vinavyohudumiwa na kituo hiki vipo mbali na miundombinu ya barabara
si mizuri, yaani hakuna usafiri zaidi ya bodaboda ambazo lazima zitoke
Simambwe…sasa kutokana na hali hii inatokea mjamzito anajifungulia nyumbani kwa
msaada wa wakunga wa jadi, akipeleka mtoto huyo kituo cha afya basi wanamuomba
shilingi 2000 haijulikani ya nini, sasa hili si tunaamini sio haki,” alisema
mama huyo.
Aidha baadhi
ya wanakijiji walikilalamikia kituo hicho kwa kitendo cha kulalamika muda wote
hakina dawa huku wahudumu wakiwaelekezwa kwenda kununua dawa jambo ambalo
wanahisi kuna mchezo mbaya unafanywa na wahudumu hao.
“Muda wote
ukienda kutibiwa utasikia kauli za hakuna dawa tunakuandikia nenda kanunue,
tena wengine wanaelekeza hadi maduka ya kununua dawa hizo ndio maana baadhi
yetu tunahisi kuna mchezo mbaya (kuhujumu dawa) unaofanywa na baadhi ya
wahudumu.,” alisema Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Kalamwa.
Kwa upande
wake Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo alipinga vikali uwepo wa vitendo vya kuomba
rushwa kwa watumishi wa kituo hicho na kudai malalamiko kwa wanachi
wanaohudumiwa na kituo hicho imekuwa kitu cha kawaida hasa wanapotembelewa na
mgeni.
“..Hakuna
kitu kama hicho unajua wakazi wengi wa vijiji hivi wamezoea kulalamika hasa
wanapotembelewa na mgeni…hakuna wanaoombwa fedha, mjamzito akijifungua nyumbani
tunampokea bila masharti na kumpatia huduma anazostahili, si kweli
wanachokilalamikia,” alisema Mwaipopo.
Hata hivyo
alisema kituo hicho kinahudumia idadi kubwa ya watu zaidi ya uwezo wake jambo
ambalo hukifanya kuelemewa kwa idadi ya dawa wanazoletewa, wahudumu na vifaa
vingine tiba hivyo kuiomba Serikali kukiongezea mgao wa dawa.
“…Kituo
kinahudumia idadi kubwa ya watu kupita uwezo wake hivyo unakuta hata baadhi ya
changamoto kama ufinyu wa dawa na wahudumu vinatokana na hali kama hiyo…,”
alisema Mganga huyo Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe.
*Imeandaliwa
na www.thehabari.com kwa ushirikiano na
TGNP
Wizara sikia kilio hiki na mchukue hatua ondoa hawa corrupt staff, watu wapo mtaani hawana kazi weka hapo!
ReplyDelete