Saturday, April 19, 2014

WaTanzania Wako Wapi Katika Mbio za Kukimbia Siku Hizi?

Wadau, mnakumbuka majina, Suleiman Nyambui, Juma Ikangaa, Filbert Bayi, Nzael Kyomo,  Walikuwa wanariadha walioshinda katika Marathon na  michezo Olympics.  Walifanya jina la Tanzania ijulikane na isifike! Waliinua jina la Tanzania.  Lakini kwa sasa mbona Tanzania haijawa na mwanariadha anayeweza kushinda  kwa miaka mingi?

Jumatatu kutakuwa na mashindano ya Boston Marathon. Karibu kila mwaka ni MKenya anayeshinda! Kenya ni nchi jirani na sisi, kwa nini Tanzania hatuwezi kushinda? Au tabia ya Party kila wiki na mkao wa kula/bahasha umefanya watu wasijali.

Kwa habari zaidi za KUZOROTA KWA MICHEZO TANZANIA, BOFYA HAPA:

************
Suleiman Nyambui - Alishinda Tuzo ya Fedha (Silver) katika Commonwealth Games huko akiwa amefunga kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhan!  BOFYA HAPA kwa habari zaidi



Suleiman Nyambui akifanya mazoezi Texas, USA
********************

Nzael Kyomo  alishiriki Olympics mwaka 1980 halafu alienda kusoma Marekani.  BOFYA HAPA:


********************

Juma Ikangaa alishinda Marathon nyingi ikiwemo New York Marathon.  Alipata zawadi ya Benzi ambayo serikali ya Tanzania walizuia bandarini kwa zaidi ya mwaka kwa vile Ikangaa hakuweza kuilipia ushuru! Aibu kwa serikali kumnyanyasa shujaa!  BOFYA HAPA:  

Juma Ikangaa katika Boston Marathon 1990

****************************

Filbert Bayi alishinda mashindano ya Olympics na Commonwealth Games.   Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Filbert Bayi katika mashindano ya Commonwealth 1974

2 comments:

  1. What is kula bahasha? Indeed, it's sad about Tanzania runners. Maybe it's a case of not having good coaches and proper facilities, as the Tanzanian government doesn't attach much priority to expenditure on sports and athletics these days?

    I suppose TALENTED kids are still there... It's just a case of nurturing and encouraging talent.

    ReplyDelete
  2. chama cha riadha tanzania hakipo imara kwa sasa

    ReplyDelete