Sunday, June 15, 2014

Mh. Samuel Sitta Akutana na WaTanzania Cambridge, MA

Mh. Samuel Sitta akiwa nyumbani kwangu Cambridge, MA, USA
Siku ya jumamosi, 6/15/14 jioni, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba na Waziri wa Afrika Mashariki​​, Mheshimiwa Samweli Sitta alikutana na baadhi ya viongozi wa Jumuiya za waTanzania wa New York na Massachusetts. Mkutano ulifanyika Cambridge, Massachusetts.  Katika mkutano huo Mh. Sitta aliongea kuhusu maswala ya Katiba na Uraia Pacha.  Pia aliongea kuhusu jinsi waTanzania wa diaspora watakavyoweza kusaidia kuijenga Tanzania. Mh. Sitta alikuwa Boston kwa ajili kozi fupi katika Chuo Kikuu cha Harvard.

Kwa picha na habari zaidi tembelea VIJIMAMBO BLOG. 


Kutoka Kushoto - Mr. Sangiwa, Mr. Temba, Dr. Malima, Mh. Sitta, Mr. Sangiwa, Mr. Tome, Mr. Mhellla, Chemi
Mh. Sitta akiwa mwingi wa furaha baadaya kuongea na WaTanzania mjini Cambridge, MA


8 comments:

  1. Walichokifanya was really unfair. Ilikuwa Watanzania wote tujulishwe na tufanye like town hall meeting ili tuweze kumuuliza maswali muhimu ya namna anavyoliendesha hilo Bunge la Katiba. Nawashangaa Watanzania pamoja na kuishi Nchi zenye highly freedom of expression and integrity and human rights bado wanaendekeza Bureaucracy ya hali juu.

    ReplyDelete
  2. Mimi nawapongeza viongozi kutuwakilisha. Suala la uraia pacha ni letu wote. Hata wewe unayelalamika peleka malalamiko yako kwa mbunge wako ili alitetee suala la uraia wa nchi mbili.

    ReplyDelete
  3. Mimi nasema hivi, wacheni kulalamika. Malalamiko ya nini? Ujumbe umefika na suala la uraia linasonga mbele. Asante Baba Sitta kwa kuwasikiliza viongozi wetu. Tunaelewa kiongozi hawezi kumpendeza kila kila mtu na hawezi kupendwa na wanajumuiya wote. Kazi wanayoifanya viongozi wetu ni nzuri na Mheshimiwa Sitta fahamu ya kwamba tunawaunga mkono viongozi wetu na wametuwakilisha na tunakushukuru kwa kukutana nao na kwa kuwasikiliza.

    ReplyDelete
  4. Nyinyi bishaneni, mimi na Tanzania yangu tu. Naipenda Tanzania. Nawapenda Watanzania. Mheshimiwa Sitta asante sana baba kwa kukutana na Watanzania na wanadiaspora. Tunakukaribisha Texas ukija tena ili nasi tukuone.

    ReplyDelete
  5. Katibu wetu tunakupongeza kwa kazi yako nzuri unayoifanya licha ya hao wanaokuzunguka kuwa na mbwembwe nyingi za kukupaka matope. Na huyo anayekulaumu ni mmojawapo wa wale wanaokuzunguka na kukupaka matope ili uonekane hufai. Lakini kazi yako tunaiona. Mwacheni Katibu wetu afanye kazi yake. Endelea na kazi hao wanaokupiga zengwe ni kama mbwa waoga ambao hufoka kwa kubweka sana na ukiwakaribia utimka mbio. Fanya kazi kijana achana na hao wasiopenda maendeleo.

    ReplyDelete
  6. Hivi nani kama Kikwete? Maana baraza lake la mawaziri linachapa kazi sana. Na kama matatizo yapo ni kawaida kwa kila nchi. Huyu Sitta ni kiongozi shupavu na mpenda haki. Tutendee haki baba watoto wetu wapate uraia pacha. Tunatanguliza shukrani zetu kwa Mheshimiwa Rais Kikwete na kwa Mheshimiwa Sitta vile vile kwa kukutana na viongozi wetu.

    ReplyDelete
  7. Badala ya kuwalalamikia viongozi kwenye mitandao, hamuwezi kuwatafuta na kuwakilisha manung'uniko yenu kwa viongozi wenu, uso kwa uso? Kuweni wastaarabu na msichafue hali ya hewa kwenye habari nzuri kama hii bila sababu yeyote.

    ReplyDelete
  8. Looking good as usual, Da Chemi.

    ReplyDelete