Thursday, January 01, 2015

Mhabusu Auwawa Mahakama ya Kisutu

MAHABUSU AUWAWA KWA  RISASI MAHAKAMA YA KISUTU AKIJARIBU KUTOROKA

Na Happiness Katabazi

JESHI la Magereza limefanikiwa kumdhibiti Mahabusu  wa Kesi ya dawa za kulevya ambaye ni Raia wa Sieralioni,  Abdul Koroma (33) asitoroke chini ya Ulinzi wa Askari Magereza ndani  Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkazi Kisutu Dar es Salaam, asitoroke chini ya Ulinzi  baada ya kumtwanga risasi na kumuua papo hapo.

Wakizungumza na mwandishi wa Habari hizi baadhi ya wanausalama waliopangwa kulinda Usalama Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa Masharti ya kutotajwa Majina Yao kwa Madai wao siyo wasemaji wa majeshi Yao wakisema mtuhumiwa ambaye anashitakiwa kwa makosa ya kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya Heroin Zenye uzito wa Gramu 1229 na zenye thamani ya Zaidi ya Sh.Milioni 61 iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alistahili kufanyiwa hicho alichofanyiwa.

Walisema Asubuhi marehemu Huyo ambaye ni mahabusu aliletwa na mahabusu wenzake na Askari Magereza na Kisha kufikishwa Katika mahabusu ya Mahakama hiyo mtuhumiwa aliomba apelekwe chooni kujisadia lakini ghafla mtuhumiwa akaanza jaribio la kuparamia ukuta akimbie ndiyo Askari waliokuwa akimsikindikiza chooni wakafyatua risasi hewani ili kumtaka aache ili jaribio lake lakini Inadaiwa Koroma aliendelea na jaribio lake.

" Ndipo itabidi mmoja wa Askari Magereza 'ameshone risasi' yaani amefyatulie risasi Koroma ambayo ilimpata na kumsababishia mauti papo hapo ....na baada ya Koroma kupekuliwa wanausalama Hao walipokuwa soski walikuta ndani ya soksi alilovaa kuna kikaratasi kilichochorwa ramani na namba za simu za watu wa kumpokea haoa Dar es Salaam" kilisema chanzo changu.

Tayari mwili wa Koroma ambaye alikuwa akikabiliwa na Kesi yake P121/2013 umeishaondolewa Katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umepelekwa kuinadi wa Katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 31 Mwaka 2014.


Kisutu Court Dar es Salaam


No comments:

Post a Comment