MUNGU AKULINDE SOSPETER MUHONGO
Na Happiness Katabazi
LEO saa
tano asubuhi, Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo alitangaza rasmi kujiuzuru nafasi hiyo ya uwaziri kwasababu ya
zogo la Escrow.
Tangu mwanzo kupitia makala yangu msimamo wangu
niliweka wazi Kuwa naunga mkono Utendaji kazi wa Profesa Muhongo na hata
Leo hii ninavyoandika makala hii sitabadilisha msimamo wangu Kuwa
Kwangu Profesa Muhongo ni Miongoni mwa Mawaziri wa Nishati na Madini
ambao nimewashuhudia Kuwa ni mawaziri ambao wameacha alama ya
kukumbukwa.
Pia tangu mwanzo nilisema wazi kupitia makala zangu
mbalimbali kwa jicho la Sheria Katika zogo la Escrow Hakuna Mashitaka ya
wizi Kama baadhi ya watu walivyokuwa wakiwa hukumu Moja kwa Moja watu
waliotajwa kwenye zogo la Escrow Kuwa ni wezi na kwamba Fedha za Escrow
zimeibwa.
Hoja yangu ilipingwa na baadhi ya watu waliokuwa
wakisema Fedha za Escrow ni za umma na fedha hizo za Escrow zimeibwa na
waliiba ni wezi wanastahili kushitakiwa kwa wizi, ilikuja Kufungwa mkono
na Rais Jakaya Kikwete, Disemba 22 Mwaka Jana, Katika mkutano wake na
wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na mengine alisema hatukuwa na
wizi Katika Fedha za Escrow na Fedha za Escrow siyo mali ya umma.
Pia
mapema Mwaka huu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ili
wafungulia Kesi ya kupokea Rushwa kutoka kwa Lugemalila baadhi ya
maofisa wa serikali ambao waliotajwa kwenye zogo la Escrow.
Tusubiri
hatima ya Kesi hizo itapofika Tamati na tusubiri pia ushahidi
utakaotolewa na Huyo Lugemalila je Lugemalila akifika mahakamani atatoa
ushahidi wa ni kweli au si kweli aliwapa rushwa? pia tusubiri utetezi
wa washitakiwa hao na uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam, utakapotolewa.
Profesa Muhongo ametaja baadhi ya Sababu
zilizomsukuma kufikia uamuzi huo, Nampongeza kwa uamuzi huo licha
amekuchukua wakati Tayari mashankupe na mapashukuna wameishalipaka
matope jina lake Mbele ya Jamii.
Waswahili wanasema penye ukweli,
uongo ujitenga. Hivyo ipo siku ukweli wa hili zogo la Escrow utakuja
kujulikana nani muhasisi wake? Kwanini waliliasisi zogo hili?,Muhongo
alishiriki kwa kiasi gani Katika jambo Hilo?Ni kweli Katika Utawala wa
Muhongo Wizara ya Nishati ilipata Hasara na kwamba Hakuna jambo lolote
la maendeleo alilolifanya?
Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa
wakati akitoa hotuba yake bungeni wakati ajijuzuru pamoja na mambo
mengi alisema ; ' Tukiruhusu kila mwanasiasa ajijuzuru kwa tuhuma tu
ambazo hata hazijathibitika Hakuna mwanasiasa atakayebaki salama'.
Kweli sasa mantiki ya ubashiri huo wa maneno ya Mzee Lowassa yameanza kutimia.
Hongera
Muhongo kwa uamuzi huo Kwani utakupa fursa ya kwenda kufanya shughuli
nyingine kwa Amani na utulivu kwa watu wenye akili timamu ambao
wanamisimamo usiyoyumba na Kamwe hawaamini katika majungu na upashukuna.
Mema
uliyoyafanya Katika Wizara ya Nishati na Madini,tutayakumbuka na
tutaheshimu mchango wako katika sekta ya nishati na madini.
Utendaji
kazi wako kumbe ulikuwa ukiwakera baadhi ya walafi .Na watu wanaofikiri
sawa sawa tunajiuliza ni kwanini kila kukicha Mawaziri wa Wizara ya
Nishati na Madini hasa katika serikali ya awamu ya nne wamekuwa
wakishambuliwa wazi wazi na mwishoe wamekuwa wakijiuzuru au kuondolewa
katika wizara hiyo?
Mbona Wizara Kama Wizara ya Maendeleo ya
Jinsia na Watoto hata siku Moja hatushuhuudii wanasiasa uchwara
wakikomalia Kuwa mawaziri wake wameshindwa kazi Kwani kila siku ripoti
zinaonyesha watoto wadogo ,wanawake wanafanyiwa vitendo Vya kikatiri
Kama kubakwa na Kuuwawa?
Ni Wizara ya Nishati na Madini tuu ndiyo
inastahili kumulikwa ? .Jibu ni Jepesi hapa ni manyang'au yenye Nguvu
za kifedha yalizibiwa mirija ya kufanya biashara zao kwa njia chafu
Katika sekta ya Madini na Nishati.
Ikumbukwe Kuwa wale wote ambao
mnatumia Hiari na uchafu wa kila aina kuwachafua wenzenu na kuakikisha
wenzenu wanatoka madarakani kwaajili ya mashinikizo yenu, ipo siku na
Nyie wakati wenu utafika wa kulipwa hapa hapa na Mungu malipo ya hizo
hira Zenu na msije kulia na Mtu.
Nchi hii Ilipofika hivi sasa,
majungu, fitna,ushirikina, uzandiki Ndio umetawala na umeshika
hatamu.Watu wasiyo na hatia na siyo kwenye Nyanja za siasa tu
wanaangamia kwa ushenzi huo.
Imekuwa nchi ya watu tunaopenda
Ujinga Ujinga na uzushi halafu na mbaya zaidi tabia hizo zinafaywa na
wanaume amba wanawake nyumbani eti tunajiaminisha nchi hii itapata
maendeleo kwa haraka.
Wito wangu kwa Watanzania wanaishi nchi za
nje na kufanya kazi katika taasisi za kimataifa nje ya nchi na wamesoma
vizuri ,wasiwe wepesi sana kurudi nchi Kuja kufanyakazi Hasa za kisiasa
kwa kisingizio eti serikali imewaomba sana Kuja Tanzania kufanya kazi.
Nawaomba
mjifunze kwa yaliyowakuta wenzenu ambao walikuwa wakifanyakazi nje ya
nchi akiwemo Profesa Muhongo ambaye alikuwa akifanya kazi nje ya nchi,
serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakyaa Kikwete ikamuona wa maana
sana, ikamtaka arejee nchini aje alitumikie nchi na kweli alikuja
kuitumikia lakini malipo aliyoyapata ndiyo hayo mmeyaona.
Ambayo
minayafananisha na tabia zinazofanywaga na waswahili swahili huku mtaani
za kumkodishia ngoma ya mdundiko mtu na kuja kumsuta mtu.
Au
kumkodishia mapashukuna kila kukicha wawe wanamchafua jina lake na
kweli wamefanikiwa na waliokuwa wanatakiwa wadhibiti Hali hiyo wamekaa
kimya.
Mke wangu IGP- Said Mwema na Mkurugenzi wa TAKUKURU
,Dk.Edward Hosea wakati Sakata la Fedha za EPA bado washitakiwa
hawajapelekwa Mahakamani na wananchi walikuwa wakishinikiza wapelekwe.
Viongozi
Hao ambao ni makachero wazuri tu walikuwataka wananchi wawe na subira
na Kusema HIvi " Mafisadi ni watu hatari sana hivyo inatakiwa kwenda nao
Polepole". Ni kweli makachero hao walikuwa walikuwa wakijua
wanavyosema na ndicho kilichomkuta Mtani wangu Muhongo.
Hivyo
Muhongo muachie Mungu, yeye ndiyo muweza wa yote, endelea kulitumikia
taifa Lako kwa uaminifu ila kwa taadhari pia Kwani Tulipofika sasa
watendaji waaminifu na wachapakazi nchi hii HIvi sasa nikama hawatakiwi.
Tusubiri
tuletee Waziri wa Nishati na Madini ambaye uenda anaweza Kuwa malaika
kutoka mbinguni ambaye Kamwe hataguswa na tuhuma yoyote Kama watangulizi
wake Wizara hiyo walivyokabiliwa na tuhuma na kutakuwa kujiuzuru.
Pia
tusubiri Huyo Waziri wa Nishati na Madini mpya ambaye atateuliwa na
Rais Kikwete ambaye ataweza kuendeleza Yale yaliyoachwa na Muhongo na
alete mipango yake Mipya Katika Kipindi hiki kifupi kilichobakia
kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka 2015. Na tumpe ushirikiano siyo
kuanza kumchokona.
Mwisho namtakia kila la kheri Mtani wangu
Profesa Muhongo Katika majukumu yake mapya.Hongera kwa uamuzi huo wa
kujiuzuru licha kwa wale walikuwa tunafahamu mchango uamuzi huo
umekusikitisha ila hatuna jinsi.
Wewe siyo wa kwanza kujiuzuru
nafasi hiyo kwa Sababu umeona jina Lako lime nafika. Hata aliyekuwa
Waziri wa serikali ya awamu ya Tatu, Dk. Kitine naye Alifikia uamuzi wa
kujiuzuru uwaziri kwa Madai Kuwa alitafuna Fedha za umma kwa kisingizio
Kuwa Mkewe alikuwa Amelazwa Canada kwaajili ya matibabu na Katika
mahojiano yake na Gazeti la Mtanzania la Jumapili la wiki iliyopita ,
Dk.Kitine akifanya mahojiano na Gazeti Hilo alilitaja kundi la
wanamtandao na ndiyo walioshiriki kumzushia fitna hiyo na walifanikiwa
kumchafua kwasababu walikuwa wakiisoma Rais Benjamin Mkapa alikuwa
akimwandaa Kuwa Rais wa Tanzania Mwaka 2005.
Lakini Kamati ya
Bunge ya Wizara ya Mambo ya nje ilikuja kumsafisha na kunekana ni kweli
Mke wake alikuwa ni mgonjwa na alilazwa huko Canada.
Narudia
tena wale wote mabingwa wa kufanya binadamu wenzao kwa Lengo tu la
kupata maslahi Fulani ikiwemo biashara, vyeo Mkae mkijua ipo siku Mungu
atawaadhibu.
Kumbukeni hawa mnao wafanyakazi ufedhuli nao wana
Mungu na Mungu wao wala siyo kipofu wala kiwete anayetembelea
Magongo.Ipo siku Mtalipwa Ubaya mnaofanyia wenzenu.Aminini hivyo.
Mungu akutangulie Muhongo nenda kafanyekazi na wasomi wenzio achana na
hawa wanaume 'wachambue Michele' ambao wametawaliwa na husuda na fitna
na unafki na vichwa vyao wanavitumia kwaajili ya Kufugia nywele badala
ya kufikiri.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Januari 24 Mwaka 2015
0716 774494.
No comments:
Post a Comment