Saturday, February 28, 2015

Historia Fupi ya Marehemu Captain Komba!

 Mbunge wa Mbinga na Msanii maarufu, Captain John Komba, alifariki dunia leo katika hospitali ya TMJ mjini Dar es Salaam, kutokana na athari za ugonjwa wa kisukari. Mwenyezi mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
The late Captain John Komba


Historia Fupi ya Marehemu John Komba
Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1954 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1977 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.


**********************************************************************

Waziri wa Ardhi,William Lukuvi (wa kwanza kushoto) akimfariji mke wa marehemu, Salome Komba

Khadija Kopa akilia kwa Uchungu nyumbani kwa Komba.
 

5 comments:

  1. Ana 70!!!! Na mbona alimwambiaga warioba kazeeka awaache vijana ambao ndo kama yy ndo wanajua katiba itakuaje!!!??? Makubwa!! ........basi vyeti vya kazi vitakua vinaonyesha umri tofauti.

    ReplyDelete
  2. Mungu kamuwahisha nilipenda aishi maisha marefu aone majigambo yake kuwa yalikuwa si lolote wananchi tulikuwa tunamuona hana point alipoongea bungeni na pia ajue kuwa warioba hakuwa saizi yake. Ila kazi ua mungu haina makosa

    ReplyDelete
  3. Mungu kamuwahisha nilipenda aishi maisha marefu aone majigambo yake kuwa yalikuwa si lolote wananchi tulikuwa tunamuona hana point alipoongea bungeni na pia ajue kuwa warioba hakuwa saizi yake. Ila kazi ua mungu haina makosa

    ReplyDelete
  4. Mininaweza kusema hata kama alifanya matendo yanayoonekana katika jamii ni mabaya sio sababu ya kifo chake! Isipokua siku ikawadia hata ungekuwa mwema kiasi gani mauti ni lazima, hivyo kwa wema na upendo wa MUNGU kwa njia ya KRISTO atamsamehe pale aliposhindwa kutimiza wajibu wake na hatimae KRISTO arudipo akawe miongoni mwa wale waingio katika uzima wa milele.

    ReplyDelete
  5. Huwa hatupendi kushabikia mauti wala kufurahia kifo cha mtu ila malipo ya kila kitu yapo hapa hapa duniani

    Mshukuru Mungu kwa kila hatua na ukumbuke cheo ni dhamana usije kukitumia vibaya,

    fikiria mzee warioba yupo hai ila kapten komba katangulia mbele za haki nways RIP kaptn komba sisi sote twaja

    ReplyDelete