Albino wazusha vurugu Ikulu ya Dar es Salaam Magogoni
Vurugu
zilizofanywa na baadhi ya walemavu wa ngozi Albino katika Ikulu ya
Tanzania zimesababisha kuahirishwa kwa kikao kati ya viongozi wao na
Rais Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete alikuwa akitarajiwa kufanya
mkutano na viongozi wa Albino Tanzania TAS aliowaalika kuzungumzia hoja
zao kutokana na mauaji ya walemavu hao yanayoendelea nchini humo.
Lakini heka heka iliyotokea katika eneo la mapokezi iliwalazimu maafisa wa Ikulu kuwatawanya walemavu hao.
Ni
muda mfupi baada ya ukaguzi kuanza kufanyika katika moja ya lango la
kuingilia Ikulu, kundi moja la walemavu hao waliokuwa katika moja ya
chumba wakaanzisha malalamiko kwa sauti huku viongozi wao wakiwa
wanajiandaa kuruhusiwa na kuingia ndani.
Kelele hizo na mabishano
hayo miongoni mwa walemavu hao kwa mbali ikaanza kuonekana ni dosari
namba moja hasa baada ya kupandisha mori na kila mtu kuanza kusema lake
kupinga ushiriki wa viongozi hao.
Kutokana na vurugu hizo
maafisa wa Ikulu waliwatawanya Walemavu hao kutoka nje ya Geti, na hapo
ikawa mwanzo wa sakata jipya baada ya kuanza kulumbana na viongozi wao
na hatimaye kuanza kupigana na mambo yakawa hivi.
Baada ya
kutulizwa ugomvi kilichofuata ni nyimbo za kupinga uhalali wa viongozi
wao. Hata hivyi vurugu hizi zinatazamwa tofauti na baadhi ya walemavu
hao, ambao wanasema ni vurugu hizo zimepoteza fursa ya kuwasilisha
matatizo yao kwa Rais
Chanzo: BBC swahili
--
No comments:
Post a Comment