Tuesday, March 31, 2015

Tanzia - Dr. Aleck H. Che-Mponda, Baba yangu mzazi

Wadau, ninasikitika kutangaza kifo cha Baba yangu mzazi, Dr. Aleck H. Che-Mponda, kilichotokea katika hospitali ya Massana mjini Dar es Salaam, jana jioni (March 30, 2015).  Mipango ya mazishi inafanyika.  Alikuwa anumwa ugonjwa wa Saratani (Cancer ya Mifupa).

Habari ziwafikie ndugu na marafiki wote popote walipo.

Rest in eternal peace, Dr. Aleck H. Che-Mponda (1935-2015)





21 comments:

  1. Rest in peace Mzee wetu. Pole Dada Chemi na wanafamilia.

    ReplyDelete
  2. Chemi, Kwa niaba ya Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika familia ipokee rambi rambi zetu za dhati. Professa alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Idhaa hii mwaka 1962, na aliendelea kuwa rafiki mkubwa wa Idhaa. Sisi wa leo tusingekuwa hapa kama sio yeye - Mwamoyo Hamza

    ReplyDelete
  3. Pole sana dada Chemi. Mungu awape wepesi katika wakati huu mgumu na ampe mapumziko mema mzee wetu

    ReplyDelete
  4. Pole sana. May his soul rest in eternal peace.

    ReplyDelete
  5. Pole da Chemi! Nimepata taarifa toka kwa binamu yako Marry Haule wa Kibaha

    ReplyDelete
  6. Poleni sana wanafamilia, namkumbuka sana kwa msaada wake wa ushauri kwa watoto yatima. Mungu ailaze vema roho yake peponi, AMEN

    Andrew Mwansumbule Jackson

    ReplyDelete
  7. Pole sana dada Chemi..Mwenyezi Mungu aiweke roho ya babatu pema peponi. Amina

    ReplyDelete
  8. Rest in peace babu. Mungu atupe nguvu wote katika kipindi hiki kigumu.

    Harieth Lumbanga Matlou

    ReplyDelete
  9. Chemi, sorry to hear about your dad.
    I will forever be grateful for the hospitality him and your mom showed us whe we invaded your house filming Bongoland II few years ago. May God rest his soul in Peace! Josiah K

    ReplyDelete
  10. Pole sana dada chemi, Mungu ampumzishe kwa amani mzee wako. sikumfahamu baba yako lakini kutokana na picha nyingi ulizozipiga wewe, mama yako na baba yako zinatuonyesha alikuwa ni mzazi aliye jali familia yake. Mungu ampokee kwa amani. Amina
    James B.Kalugira.

    ReplyDelete
  11. Pole sana Chemi, mola akufariji kwa kuondokewa na baba yako mzazi. Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi.

    ReplyDelete
  12. Pole sana Chemi, mola akufaraji kwa kuondokewa na baba mzazi. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu.

    ReplyDelete
  13. Pole sana dada Chemi na familia yote.
    Mungu ampe pumziko la Milele.

    ReplyDelete
  14. Naitakia Familia ya Chemponda Pole kwa kumpoteza mzee wetu. MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MZEE WETU AMEN.

    ReplyDelete
  15. Dada Chemi, Nimesikitishwa sana na taarifa za kuondokewa na baba yako mpendwa, mwanasiasa na msomi ambaye alitoa mchango uliotukuka si kwa nchi ya Tanzania tu bali ulimwengu mzima kwa ujumla. Tafiti zake, pamoja na makala mbali mbali umekuwa mchango mkubwa kwenye tasnia ya siasa na elimu kwa ujumla. Nawaombea kwa mwenyezi Mungu ili aweze kuwa pamoja nanyi hususani katika kipindi hiki kigumu. Bwana alitoa na bwana ametoa jina lake litukuzwe.

    ReplyDelete
  16. Pole sana Da Chemi. Tuko pamoja katika kuomboleza msiba wa Dr Aleck Che Mponda.

    ReplyDelete
  17. Sincere heartfelt CONDOLENCES to Chemi, family and friends. May Dr Aleck Che Mponda REST IN PEACE.

    ReplyDelete