Nilifanya kazi nao wapiga picha nikiwa mwandishi wa habari Daily News miaka ya 1980's! Enzi zile tulikuwa wachache na wote tulijuana. Mzee Makwaia alikuwa Mwalimu wetu TSJ. Alifariki tukiwa mwaka wa kwanza baada ya kugongwa na gari Morogoro Road.
Kwa hisani ya Kaka Juma Dihule:
WAFAHAMU WAPIGAPICHA WA VYOMBO VYA SERIKALI ENZI HIZO.
Wapigapicha
wa wakati huo ambapo vyombo vya habari vilimilikiwa na Serikali pamoja
na chama tawala. Waliosimama nyuma toka kushoto marehemu Max Madebe
(Mpigapicha Mkuu gazeti la Mfanyakazi, Marehemu Sam Mbando, mpigapicha
mwandamizi Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA), Marehemu Vincent Urio
(Mpigapicha Mkuu magazeti ya Serikali ya Daily News & Sunday News,
Marehemu John Makwaia ndiye aliyekuwa mwalimu wetu sisi wote na
mpigapicha mkuu wa Serikali katika Idara ya Habari (MAELEZO),
akifuatiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye pia ni
marehemu, David Saileni ambaye wakati huo akiwa mpigapicha mwandamizi wa
Sinema, upande wa Idara ya Habari, (Film Unit), Juma Dihule,
Mpigapicha Mkuu SHIHATA, Marehemu Adnani Mihanji, Mpigapicha
Mwaandamizi, SHIHATA na Moshy Kiyungi, Mpigapicha mwandamizi ( Idara ya
Habari).
Walioketi toka kushoto, Steven Kasange, IKULU, Charles
Kagonji , Mkutubi Mkuu wa maktaba ya picha MAELEZO na pia akiwa
mpigapicha, Gaspar Msilo, Daily News, Mwanakombo Jumaa, MAELEZO, Hatib
Ali Mpichapicha Mkuu (Uhuru na Mzalendo) Raphael Hokoro , ambaye hivi
sasa ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO).
Dada Chemi
ReplyDeleteUmenikumbusha mbali. Miaka ile ya themanini na kurudi nyuma, ninayemkumbuka sana ni Vincent Urio. Kwangu alikuwa kama alivyo Freddy Maro leo au Muhiddin Issa Michuzi. Moto wa kuotea mbali.