Sasa amefariki mh. Deogratius Haule Filikunjombe. Duh! Amefariki katika ajali ya Helikopta katika mbuga ya wanyama ya Selous. Alikuwa akitokea Dar kwenda Ludewa kwenye shughuli za kampeni. Katika ajali hiyo amekufa rubani wa helikopta hiyo Capt. William Silaa, ndugu wa Filikunjombe, Plasdus Haule, na mfanyakazi wa Halmashauri ya Ludewa. Mtoto wa rubani alisema kuwa helikopta hiyo ilipata matatizo ya injini kabla ya kuanguka kwake na kuteketea kwa moto.
Mwenyezi mungu alaze roho zao mahal pema mbinguni. Amen.
Close-up (Picha ya karibu) ya helicopter aliyokuwa anatumia Mh. FIlikunjombe kwenye shughuli za kampeni. |
Mwili wa Deo Filikunjombe ukitolewa Eneo la tukio baada ya kuteketea kwa Moto kufuatia ajali ya helkopta. |
Mabaki ya Ajali ya Helicopter. Mh. Deo Filikunjombe na wengine watatu walifariki katika ajali hiyo Selous Reserve |
Mabaki ya Ajali ya Helicopter. Mh. Deo Filikunjombe na wengine watatu walifariki katika ajali hiyo Selous Reserve |
Rubani Maarufu Captain William Silaa (enzi za uhai wake) ndiye alikuwa anaendesha helicoopter hiyo |
Helicopter Aliyokuwa anaitumia Mh. Deo Filikunjombe ikiwa anagani |
Helicopter aliyokuwa anaitumia Mh. Deo Filikunjombe |
Mh. Deo Filikunjombe (enzi za uhai wake) akiaanga na wananchi wa Ludewa |
Mh. Deogratius Filikunjombe (1972 -2015) |
Leo nimeelewe wa Tanzania walivyojisikia 12/04/ 1984 alipo fariki Sokoine. Deo Filikunjombe mungu wa mbinguni akupokee na fungu lako akupe, pumzika kwa amani.
ReplyDeleteAisee, hivi vifo vya wanasiasa vinatisha!!!!
ReplyDeleteWana maombi tuombe sana Mungu
Tanzania , inabidi tuombe mungu sio bure , viongozi wanakufa mfululizo , kuna mahali tumekosea kama taifa , mungu anatuonyesha
ReplyDeleteHili ni ghalika! Uwepo wa Mungu unahitajika sana.. R.I.P.
ReplyDeleteDeo umeondoka! Hakuna tena ambae atashawishi watu kuipenda ccm ww ulikuwa ni wa pekee hakuna wa kufananishwa na ww ndani ya ccm Mwakyembe, alisha potea hivyo bc ccm inazidi kuzama !
ReplyDeleteBwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe sababu ni katika kufa ndipo tunapata uzima wa milele RIP Deo.
ReplyDeleteWote tutakufa/ Kila mtu ataondoka na staili yake. Rest in peace.
ReplyDeleteWengine walikuwa kwenye timu ya operation bao la mkono.
ReplyDeletePia huyu ndugu yetu Deo Filiku hali akijua udhalimu wa ccm bado akaendelea kuwaunga mkono,basi mimi ninaamini hii ajali ni Mungu ametaka kuwaonya wale aliowapa ufunuo wa udhalimu wa CCM kwa wa-Tanzania.
Mapenzi yake yatimizwe.
Amen.
Pumzika kwa Amani Kiongozi wa kweli,hakika pengo lako halitazibika.
ReplyDeletePumzika kwa amani Deo , kazi aliyokutuma Bwana umeimaliza.
ReplyDeleteKule mwanza wenyewe wanaendelea kukata viuno.....pumzika kwa amani kamanda...poleni wana-Ludewa na watanzania kwa ujumla
ReplyDeleteDah ni pigo kubwa kwa Taifa, R.I.P. Kaptain Slaa na Jembe letu Deo Filikunjombe, tutamkumbuka daima jamani
ReplyDeleteTanzania inalia,Njombe tunalia,na Ludewa wanalia zaidi.Ndani ya miezi 6,mungu kailiza jamii ya wana-Ludewa mara tatu.Mungu katuchukulia wapendwa wetu:Dr.Alec che Mponda,Rev.Christopher Reuben Mtikila na kijana wetu,mchapa kazi na kipenzi cha watu Deogratius Haule Filikunjombe.
ReplyDeletePoleni sana Ludewa,barabara,migodi ya makaa na chuma na umeme alivyovileta Deo,mvitumie vema kwa manufaa ya maendeleo endelevu,kwenu na kwa watoto wenu,huku AKIILAZA MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MPENDWA WETU Deo Haule Filikunjombe.