Kutoka kwa mwandishi mahili Nickson Mkilanya
KWAHERI YA KUONANA RC SAID THABITH MWAMBUNGU
Amefariki
leo katika hospitali ya taifa ya muhimbili,hatunaye tena, Said Thabith
Mwambungu mkuu wa mkoa mstaaf na miongoni mwa wanasiasa wabobezi na
wakongwe katika zama hizi.
Ameripotiwa
kusumbuliwa na ugonjwa wa figo kwa siku kadhaa hata akapelekwa kutibiwa
nchini India na kurejea na nafuu ambayo pia haikupata kumrejesha katika
majukwaa ya siasa na hata hadharani.
Kuugua
huko pasipo kutajwa kuwa ndiyo sababu iliyopelekea rais Magufuli
kumhamishia ofisi ya waziri mkuu na kuahidi kumpangia kazi zingine toka
juni 26 mwaka jana lakini nafsi yangu yakiri kuwa pengine hiyo ndiyo
sababu kuu.
Alilitamka
kwa ufasaha jina lake la said said thabith mwangu enzi za uhai wake
hasa pale nilipofanyakazi naye mimi nikiwa kama mwanahabari wa
luninga,radio na hata magazeti, ni mzaliwa wa Malinyi mkoani Morogoro
ambaye kwangu mimi ni miongoni mwa wanasiasa bora,baba Bora na kielelezo
cha watu wema na wastaarabu niliopata kukutana nao.
Miongoni mwa mambo aliyoyaacha km funzo kwangu ni uvumilivu na upendo. Wakati mmoja akiwa mkuu wa wilaya kuna kiongozi mmoja alimfanyia figisu figisu nyingi ambazo hata wanahabari tuliona na kugundua akionewa dhahiri! Lakini tulipoongea naye jibu lake alijibu kuwa mwacheni tu huyo, hayo ni yakupita, hajui siasa, vumilieni yataisha na kweli huyo mtu alikuja ondolewa ktk nafasi na kumwacha mwambungu akitamba na siku chache baadae kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa ruvuma.
Jambo
lingine alijua kuthamini watu na kuwaonesha upendo wa dhati hata wale
ambao kwa tabia za kibaguzi wasingepaswa kumsogelea lkn bado aliwapa
nafasi sawa na wale ambao kimtazamo walikuwa na sifa ya kumsogelea.
Nakumbuka wakati mmoja aliniambia nick mwanangu fanya mpango uoe
nikufanyie sherehe kabla sijaondoka na hapa alimaanisha kabla
hajahamishwa kituo cha kazi nami nilicheka na kuahidi kufanya hivyo lkn
leo hatunae tena ameondoka mwambungu pasipo kushughudia harusi yangu.
Amini mungu ni mwema wanae wakiongozwa na hamidu mwambungu watashughudia harusi yangu kwa niaba yake inshallah.
Wakati
wa uhai wake alipata kuwa kada mwandamizi katika ccm, katibu wa chama
cha mampinduzi mkoa, mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa achilia mbali
nafasi zingine nyeti ndani ya nchi hii, Na ameacha watoto watatu, hamidu
said said thabith mwambungu, Khalid na Abiba S. S Thabith mwambungu na
mjane.
Mtoto mkubwa wa marehemu aitwae Hamidu Mwambungu anasema haijaamuliwa bado kama baba yao atazikwa morogoro au kwingineko.
Tangulia mtu mwema Said Said Thabith Mwambungu.
Nice article.Congratulations
ReplyDeleteRambirambi zetu kutoka idara ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Nairobi..Unaweza ukatupa katika tovuti http://kiswahili.uonbi.ac.ke/
ReplyDelete