Saturday, December 02, 2017
Mwanza Wazindua Mwongozo Kuhusu Uwekezaji wa Mkoa
MKOA wa Mwanza umefanya Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji ambao umeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
Mwongozo huo ni sehemu ya ripoti tatu zilizotokana na agizo la mkoa wa Mwanza la kutaka kuwekewa pamoja taarifa sahihi zinazogusa uwekezaji mkoani humo ili kurahisisha na kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.
Ripoti nyingine ni Fursafiche katika Viwanda (Industrialization Potentials Report), na Ripoti ya Fursa za Uwekezaji (Investment Opportunities Report) .
Akizungumza katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, Mashirika ya Umma, Sekta binafsi na mashirika ya kimataifa, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella, alisema walilazimika kuwatafuta wataalamu wa ESRF, kuwasaidia kuweka pamoja fursa zote za mkoa katika mpangilio mmoja unaobainisha fursa zilipo.
[caption id="attachment_3212" align="aligncenter" width="1404"] Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitoa hotuba ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo uliondaliwa na ESRF kwa chini ya ufadhili wa UNDP katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Mwanza.[/caption]
kwenye viwanja vya ofisi za Mkuu wa Mkoa huo jijini Mwanza.[/caption]
No comments:
Post a Comment